Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Machi, 2018

Neymar Jr
Paris Saint-Germain imelikataa ombi la Neymar kutaka aongezewe mshahara ili abaki katika klabu hiyo ya Ufaransa msimu ujao.

Rais wa klabu ya Lyon, Jean-Michel Aulas amekanusha taarifa zinazodai kocha wa klabu hiyo ya Ufaransa, Bruno Genesio aliomba kujiuzulu baada ya timu yao kutolewa kwenye Europa Ligi. (L'Equipe)

Golikipa wa klabu ya Barcelona, Marc-Andre ter Stegen amesema kuwa klabu hiyo ya Uhispania inatakiwa kuhakikisha Andre Iniesta haondoki kwenda nchini China.
 
Martin Allen amerejea katika klabu ya Barnet kama meneja kwa mara ya tano katika historia ya klabu hiyo. (Sky Sports)

Luke Shaw alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotofautiana na Jose Mourinho wakati wa mazoezi ya timu yao kabla hajaaibishwa kwenye mechi yao ya FA Cup dhidi ya Brighton.

Louis van Gaal amesema kuwa alitaka kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski wakati alipokuwa Manchester United.

Petr Cech
Petr Cech amesema hafurahishwi na kitendo cha Arsenal Wenger kumnyima muda wa kutosha kwenye mechi za vikombe. (Sun)

Bayern Munich wamesema kuwa hawatamuuza mshambuliaji wa klabu hiyo, Robert Lewandowski anayemaliza mkataba wake mwaka 2021. (Kicker)

Klabu ya Nice imekiri kuwa Mario Balotelli anaweza kuondoka nchini Ufaransa mkataba wake utakapoisha kwenye majira ya joto.

Meneja Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marota amesema kwamba mkataba wa mkufunzi wa klabu hiyo, Massimiliano Allegri bado haujaisha na hataondoka kwenda PSG kama inavyodaiwa.
  
Romelu Lukaku anaamni kuwa klabu ya Manchester United itasajili wachezaji wengi wazuri kwenye majira ya joto. (ESPN)

Manchester United wana nafasi kubwa ya kuweza kumnasa kiungo wa Sharktar Donetsk na Brazil, Fred. (Star)

Luke Shaw
Luke Shaw anatarajiwa kuondoka Manchester United kwenye majira ya joto baada ya kuvurugwa na kitendo alichofanyiwa na Jose Mourinho. (Times)

Aliyekuwa meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amesema wachezaji wengi aliokuwa nao hawakuwa wa kimataifa kipindi alipokuwa katika katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Meneja Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta amekiri kwamba  klabu hiyo ya Italia kwa sasa imemfanya kiungo wa Liverpool, Emre Can kuwa chaguo lao la kwanza kwenye majira ya joto. (Daily Mail)

Klabu ya Manchester United inatarajia kuwauza Luke Shaw, Juan Mata, Ander Herrera, Chris Smalling, Phil Jones, Daley Blind na Matteo Darmian kwenye majira ya joto. (Express)

Wolves wana matumaini ya kuipikua Arsenal kwenye mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa AC Milan, Andre Silva ikiwa kama watapanda daraja.

Mshabiki wa Manchester United wameomba uwanja ulioandaliwa kwa ajili ya mchezo wa nusu fainali ya FA Cup ubadilishwe. (Mirror)

Angus Gunn
Celtic inatazamia kumsajili golikipa wa Manchester City, Angus Gunn. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 19 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/19/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.