Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 26 Machi, 2018
Cesc Fabregas |
Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas amesema kuwa angeweza kukimbilia nafasi ya kurejea Arsenal kama mkufunzi. (Star)
Everton ina mpango wa kumsajili beki wa klabu ya Manchester United, Chris Smalling.
Xabi Alonso amesema kuwa Liverpool ina uwezo wa kuifunga timu yoyote ile kwenye Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa Tottenham, Son Heung-Min anadai kwamba Harry Kane ndiye mchezaji bora duniani.
Courtois amesema kuwa ataendelea kuwa golikipa wa klabu ya Chelsea hadi msimu ujao. (ESPN)
Inaonekana aliyekuwa meneja wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel atajiunga na Paris Saint-Germain, licha ya kuhusishwa na klabu ya Arsenal.
Timo Werner |
Liverpool inamtamani mshambuliaji wa RB Leipzig, Timo Werner, ikidaiwa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Uingereza, Jurgen Klopp anavutiwa sana na kipaji cha nyota huyo. (Bild)
Simon Mignolet amesema kuwa hataondoka Liverpool, bali ataendelea kupigania kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.
Sergio Aguero anapanga kuondoka Manchester City mwaka 2020 wakati mkataba wake utakapokuwa umeisha. (Sky Sports)
Gareth Bale anakiri kwamba anaweza kushawishika kwenda Ligi Kuu ya China, huku future yake katika klabu ya Real Madrid ikiwa shakani.
Manchester United iko tayari kumuuza Paul Pogba kwa lengo la kujiandaa na usajili wa wachezaji watakaogharimu pauni milioni 200 kutoka Real Madrid, PSG na Juventus.
Manchester United wamefanya mazungumzo na kiungo wa Napoli, Jorginho kwa lengo la kuzitibulia Liverpool na Arsenal.
Klabu ya Swansea inataka kumsajili Andy King (aliyesajiliwa kwa mkopo) moja kwa moja kutoka Leicester - lakini ikiwa tu haitashuka daraja. (Mirror)
Joe Hart |
Meneja wa Uingereza, Gareth Southgate anapanga kumwita Joe Hart kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia - lakini atakua kama msaidizi wa Jordan Pickford. (Daily Mail)
Juventus wanajiandaa kukabiliana na Manchester United kuwania saini ya kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey anayekadiliwa kuwa na thamani ya pauni milioni 35.
Adam Lallana anakabiliana na wakati mgumu kupigania nafasi ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia - Gareth Southgate pia anajiandaa kuwaacha nje Jack Wilshere, Gary Cahill na Chris Smalling.
Phil Foden na Jadon Sancho wameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza U19 kwa sababu za utovu wa nidhamu.
Kiungo anayewindwa na klabu ya Liverpool, Javier Pastore amesema hatima yake PSG itaamuliwa kwenye majira ya joto. (Sun)
Licha ya kuhusishwa na uhamisho wa kiungo wa klabu ya Bordeaux, Malcom, Bayern Munich haina mpango wa kumsajili Mbrazil huyo.
Bayern Munich haiko tayari kumuuza Robert Lewandowski licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid na Manchester United. (Kicker)
Juhudi za Arsenal na Liverpool kuwania saini ya Thomas Lemar zimeongezwa kasi, baada ya kiungo huyo wa Monaco kukiri kuwa alikata tamaa kufuatia uhamisho wake kwenda Uingereza kugonga mwamba. (Express)
William Carvalho, ambaye alikuwa anawindwa na klabu ya West Ham kwenye majira ya joto mwaka 2017, ataruhusiwa kuondoka Sporting Lisbon kama klabu hiyo itatoa ofa ya pauni milioni 39.2
Kieran Tierney |
Manchester United wamekazania mpango wao wa kumnasa beki wa klabu ya Celtic, Kieran Tierney. (Record)
Arsene Wenger amewatuhumu mashabiki wa Arsenal wabaguzi, akisema kuwa wengi wanadai aondoke kwa kigezo cha umri wake mkubwa . (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 26 Machi, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
3/26/2018 10:18:00 AM
Rating: