Loading...

Vigogo wa EPL wanaonyatia saini ya Casillas kimya kimya

Iker Casillas
Klabu nne kutoka Ligi Kuu ya Uingereza zinawania saini ya aliyekuwa golikipa namba moja wa Real Madrid, Iker Casillas.

Raia huyo wa Uhisapni ni mmoja kati ya magolikipa wenye uwezo na uzoefu mkubwa sana, akiwa na mataji matano ya La Liga titles na matatu ya Ligi ya Mabingwa aliyotwaa akiwa na Real Madrid katika kipindi cha miaka 16.

Alikuwa pia sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Uhisapani kilichotwaa mataji mawili ya Euro na Kombe la Dunia mwaka 2008-2012. Casillas aliondoka Real Madrid kwenda FC Porto mwka 2015, na Jumanne usiku mkongwe huyo alipewa heshima kubwa na mashabiki wa Liverpool kufuatia sare yao ya 0-0 kwenye Ligi ya Mabingwa katika dimba la Anfield.

Ingawa ana umri wa miaka 37, golikipa huyo anategemewa kuondoka na kujiunga na klabu nyingine mwishoni mwa msimu, huku mkataba wake ukielekea kuisha kwenye majira ya joto. But where could he head next?

Ripoti zinadai kuwa Arsenal wana mpango wa kumsajili rai huyo wa Uhisapani, huku Newcastle, Real Betis, West Ham na Liverpool pia zikihusishwa.
Vigogo wa EPL wanaonyatia saini ya Casillas kimya kimya Vigogo wa EPL wanaonyatia saini ya Casillas kimya kimya Reviewed by Zero Degree on 3/11/2018 10:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.