Loading...

Wenger ataja sababu 3 zilizopelekea Arsenal ichapwe goli 3-0 nyumbani


Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alionekana kuwa na huzuni baada ya timu yake kupoteza mchezo wake ikiwa nyumbani kwa kichapo cha bao 3-0 dhidi ya Manchester City.

Wenger alikuwa muwazi wakati akitoa maoni yake juu ya kiwango cha wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mechi yao dhidi ya Manchester City.

Leroy Sane, David Silva na Bernado waliichanganya Arsenal kipindi cha kwanza kwa kufunga magoli matatu ndani ya dakika 30 za mwanzo.

Na Wenger amekiri kwamba timu yake ilikosa hali ya kujiamini na safu ya ulinzi haikufanya vizuri katika mchezo wote mbele ya mashabiki 58,000 katika dimba la Emirates. Na alikiri kwamba waliponzwa na safu yao ya ulinzi.

Kwa mujibu wa tovuti moja ya Uingereza, Wenger alisema: “Sidhani kama tunaweza kusema magoli yao yalikuwa bora zaidi lakini tunaweza kusema mabeki wetu walikuwa wepesi mno.

“Ilikuwa ni mechi ngumu lakini inayoelezeka kwa ukweli wa kile kilichotokea Jumapili, tulipopoteza kwa Manchester City kwenye fainali ya michuano ya Carabao na hapo suala zima la matokeo ya kiwango chetu linakuingia akilini. Wachezaji waliweka bidii kubwa leo (jana Alhamisi) lakini kwa bahati mbaya beki yetu ikakosa nguvu.’

Wenger aliongeza: “Nafikiri tulijituma sana usiku huu. Tulicheza bila kujiamini, uliweza kuliona hilo wakati mchezo unaanza na tulipata malipo yake.”

Yawezakuwa Arsenal ilishindwa kujiamini kutokana na mechi yao dhidi ya Manchester City wiki moja iliyopita wakati walipochapwa goli 3-0 pia. Arsenal wamekubali magoli sita kutoka kwa Manchester City ndani ya wiki moja. Na wakati Wenger alipokuwa akielezea mchezo wao, alikiri kwamba kukosa penalti pia ilikuwa sababu mojawapo.

‘Tulihitaji penalti ili tuingie kwenye ushindani, lakini hilo nalo lilikuwa tatizo jingine. Tulipoteza kwa timu ambayo ni bora zaidi ndani ya nchi hii kwa sasa.’’
Wenger ataja sababu 3 zilizopelekea Arsenal ichapwe goli 3-0 nyumbani Wenger ataja sababu 3 zilizopelekea Arsenal ichapwe goli 3-0 nyumbani Reviewed by Zero Degree on 3/02/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.