Loading...

Arsenal, Chelsea na Liverpool kutoana jasho kwa nyota huyu wa Serie A


Arsenal, Chelsea na Liverpool zinashindana kuipata saini ya beki wa klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly, huku zote zikiwa na hamu kubwa ya kumnasa beki huyo kwenye majira ya joto.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mmoja kati ya mabeki bora zaidi katika Serie A kwa miaka kadhaa na amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Ligi Kuu ya Uingereza.

Chelsea walishindwa kumnasa kwa ofa ya karibuni pauni milioni 60 siku za nyuma na wanabakia kuwa na nia ya kumnasa raia huyo wa Senegal.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zilizotoka nchini Italia, Liverpool na Arsenal pia wamegeukia kwa beki huyo.

Vigogo wote watatu wa Ligi Kuu ya Uingereza wako sokoni kutafuta beki wa kati mpya kwenye majira ya joto na wanavutiwa na nyota huyo wa Napoli.

Kalidou Koulibaly
Hata hivyo, Koulibaly hataondoka kwa bei ndogo na anaweza kugharimu zaidi ya pauni milioni 65.
Arsenal, Chelsea na Liverpool kutoana jasho kwa nyota huyu wa Serie A Arsenal, Chelsea na Liverpool kutoana jasho kwa nyota huyu wa Serie A Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.