Loading...

Arsenal inakaribia kumsajili beki huyu kutoka Bundesliga


Arsenal inaripotiwa kuwa mstari wa mbele kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos kwenye majira ya joto.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka nchini ujerumani, vigogo hao wa Ligi Kuu ya Uingereza wanakaribia kumnasa Mgiriki huyo anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 17.5.

Mkataba wa beki huyo wa Borussia Dortmund unaisha ndani ya miezi 12 ijayo na inaonyesha kuwa klabu hiyo ya Ujerumani itamuuza mwishoni mwa msimu huu.

Mkuu wao mpya wa kitengo cha usajili, Sven Mislintat ndiye anayetia msukumo kwenye dili hilo na ana ukaribu na wakala wa beki huyo, Konstantinos Farras.

Sokratis Papastathopoulos
Kwa upande wake beki huyo kutoka Ugiriki alisema kwamba yuko kwenye mawasiliano na mawakala kwa ajili ya mazungumzo zaidi.

Arsenal wanaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kuweza kumsajili. Hata hivyo, Manchester United, Chelsea na Juventus pia wana nia ya kumsajili.
Arsenal inakaribia kumsajili beki huyu kutoka Bundesliga Arsenal inakaribia kumsajili beki huyu kutoka Bundesliga Reviewed by Zero Degree on 4/30/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.