Rais Magufuli awajibu wabunge wanaobeza serikali kukopa
Akiwa Mkoani Iringa kwenye uzinduzi wa Barabara ya Iringa – Migori iliyojengwa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika , Rais Magufuli amesema serikali inapo kopa pesa ni kwa ajili ya miradi, na mara nyingi madeni hayo hukaa muda mrefu bila kulipwa, lakini watu wanalaumu bila kuangalia faida zake.
“Barabara ya morogoro road deni lake limelipwa mwaka juzi, amelimaliza Kikwete, unaweza ukakopa leo na ukaja kulipa baada ya miaka 40 au miaka 50, madeni tunayolipa sasa hivi yamekopwa katika awamu hizo zote, inawezekana katika awamu yangu madeni ninayokopa, madeni yake yatalipwa mimi nikiwa sipo duniani, na ndio maana huwa mnawasikia wengine wanazungumza serikali inadaiwa madeni”, amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameendelea kusema .."na huwa wanasahau, wengine wameitumia barabara hiyo hiyo kwenda Bungeni, wanaitumia barabara hiyo hiyo kwa magari yao waliyoyapata au waliyokopeshwa, lakini wakishafika kule wanasema serikali inadaiwa madeni, wanashindwa kuelewa kwamba hayo madeni ni pamoja na barabara anayopita ikienda Bungeni".
Rais Magufuli awajibu wabunge wanaobeza serikali kukopa
Reviewed by Zero Degree
on
4/30/2018 09:35:00 AM
Rating: