Loading...

Baada ya kichapo cha mabao 3-0, Uongozi Singida United umeibuka na kusema yafuatayo


Uongozi wa Singida United licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar jioni ya leo, umeibuka na kusema timu kubwa imefungwa magoli mepesi.

Akizungumza kupitia kipindi cha E Sports ya EFM jioni ya leo, Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga, amesema wamekubali matokeo huku akieleza wamefungwa magoli mepesi leo.

Sanga amekubali matokeo hayo huku akikumbushia pia kuwa waliwahi kufungwa mabao 4-0 na Simba Uwanja wa Taifa hivyo wamedai kuchukulia kama sehemu ya mchezo.

Mtibwa imeibuka na ushindi huo ikiwa inasubiriwa na Simba mjini Morogoro katika mchezo mwingine wa Ligi, Jumatatu ya wiki ijayo.

Kipigo hicho kwa Singida kimekuja baada ya kuiondoa Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa changamoto ya mikwaju ya penati (4-2).
Baada ya kichapo cha mabao 3-0, Uongozi Singida United umeibuka na kusema yafuatayo Baada ya kichapo cha mabao 3-0, Uongozi Singida United umeibuka na kusema yafuatayo Reviewed by Zero Degree on 4/06/2018 05:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.