Loading...

Biashara ya nguruwe yapigwa 'STOP' Dodoma


ILIYOKUWA Manispaa ya Dodoma imezuia biashara ya nguruwe na mazao yake kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe uliobuka katika halmashauri hiyo. Kuanzia leo manispaa hiyo ni jiji.

Daktari wa Mifugo katika Manispaa ya Dodoma, Innocent Kimweri alitangaza mwanzoni mwa wiki kwamba wilaya ya Dodoma mjini ina mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

"Naweka zuio la biashara ya nguruwe na mazao yake hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo," amesema Kimweri.

Alisema kwa mamlaka aliyopewa kifungu namba 17 cha sheria ya magonjwa ya mifugo namba 17 ya mwaka 2003, anatangaza zuio la kuuzwa nguruwe na mazao yake.

Kimweri amesema, hakuna jamii ya nguruwe yoyote awe ngiri, nguruwe pori na nguruwe wa kufugwa, ataruhusiwa kuingia au kutoka nje ya eneo la wilaya ya Dodoma, pasipokuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwake.

Amesema hakuna bidhaa inayotokana na nguruwe, ikiwemo mbolea, kinyesi, mkojo na damu itakayoruhusiwa kuingia au kutoka nje ya wilaya ya Dodoma, pasipokuwa na ruhusu ya maandishi kutoka kwake.

Kwa mujibu wa Kimweri, hakuna mnyama yeyote wa jamii hiyo atakayekusanywa kwa ajili ya kuuzwa kama bidhaa pasipokuwa na ruhusa ya maandishi kutoka kwa daktari huyo.

Pia amesema uchinjaji wa nguruwe ndani ya wilaya ya Dodoma mjini, utafanyika chini ya usimamizi madhubuti wa mtalaamu wa afya za mifugo mwenye dhamana.

Wilaya ya Dodoma imekuwa ikipatwa na mlipuko wa ugonjwa huo.

Hata Juni mwaka jana, biashara hiyo ilipigwa marufuku kutokana na mlipuko kwa ugonjwa huo.
Biashara ya nguruwe yapigwa 'STOP' Dodoma Biashara ya nguruwe yapigwa 'STOP' Dodoma Reviewed by Zero Degree on 4/26/2018 01:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.