Loading...

Kocha mpya Yanga SC aja na mfumo mpya


Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana alikiongoza kwa mara ya kwanza kikosi cha Yanga kujifua zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kuvaana na Simba.

Zahera aliwasili mjini Morogoro jana ili kukiona kikosi hicho baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga kuhusiana na masuala ya kuanza kazi.

Zahera aliingia na mtindo mwingine katika mazoezi ya Yanga kwa kuwaongoza wacheza kucheza mpira kwa spidi huku akiwasisitiza wasipoteze pasi.

Mkongo huyo aliweka msisitizo huo wa kutopoteza pasi ili kumnyima nafasi adui ya kuchukua mpira.

Licha ya kuanza kukinoa kikosi hicho jana, Uongozi Yanga umesema bado hajaanza kazi rasmi kutokana na kufuatilia kibali chake cha kazi.
Kocha mpya Yanga SC aja na mfumo mpya Kocha mpya Yanga SC aja na mfumo mpya Reviewed by Zero Degree on 4/26/2018 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.