Loading...

Mama mzazi wa msanii Lady JayDee afariki dunia


Mama mzazi wa msanii wa muziki wa bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, Bi. Martha Mbibo, amefariki dunia alfajiri ya leo.

Akithibitisha taarifa hizo kaka wa Lady Jaydee ambaye pia ni msanii Dabo, amesema kwamba mama yao amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua saratani kwa muda mrefu.

Dabo amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Jet jijini Dar es salaam, na familia itatoa utaratibu wa mazishi mara baada ya utaratibu wa kuupeleka mwili hospitali kuhifadhiwa kukamilika.
Mama mzazi wa msanii Lady JayDee afariki dunia Mama mzazi wa msanii Lady JayDee afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 4/26/2018 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.