Loading...

Breaking News: Wabunge wa Zanzibar wasusia bunge kisa Muungano


WABUNGE wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaotokea Zanzibar, wamesusa na kutoka ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma, jioni hii baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuzuia mjadala kuhusu mambo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Hayo yamejiri baada ya wabunge hao kupinga mwongozo wa mwenyekiti kuwa mjadala kuhusu Muungano usiwepo kufuatia hoja ya Mbunge Frank Mwakajoka wa Chadema aliyedai kwamba Zanzibar haipati haki zake kwenye Muungano hasa kuhusu sakata la kuuza sukari Bara.

Kufuatia hatua hiyo, Mwenyekiti Mussa Azzan Zungu alilitaka bunge lisiendelee kujadili hoja hiyo ya Muungano mpaka atakapotoa majibu ya muongozo uliombwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama.

Aidha, Mbunge Saada Mkuya (CCM) amewataka wabunge kutoubeza Muungano kwani waasisi wake waliungana kwa spirit ya Umoja hivyo wasiibeze serikali badala yake waimarishe Muungano kwani una manufaa kwa pande zote.
Breaking News: Wabunge wa Zanzibar wasusia bunge kisa Muungano Breaking News: Wabunge wa Zanzibar wasusia bunge kisa Muungano Reviewed by Zero Degree on 4/09/2018 06:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.