Loading...

Guardiola atajaribu kumshawishi kiungo huyu wa Barcelona ajiunge na Man City


Pep Guardiola atajaribu kutumia uhusiano wake na Andres Iniesta kujaribu kumshawishi kiungo huyo wa Barcelona ajiunge na Manchester City, kwa mujibu wa ripoti za Uhispania.

Mkataba wa Iniesta katika klabu ya Barcelona unaisha mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda China.

Lakini imeripotiwa kwamba Guardiola atajaribu kumshawishi nyota huyo ajiunge na Ligi Kuu ya Uingereza.

Gazeti la michezo la Uhispania, AS linaripoti kwamba, meneja huyo wa Man City ana nia ya kumpa nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 nafasi ya kuendeleza historia yake ya soka nchini Uingereza.

Guardiola managed Iniesta when he was manager of Barcelona between 2008 and 2012
Iniesta amecheza zaidi ya mechi 700 akiwa na Barcelona na alichukua nafasi ya  Guardiola kwa ufanisi wakati alipoondoka katika klabu hiyo mwaka 2001.

Hivi karibuni, Guardiola alisema kwamba angeweza kusubiria aone kama Iniesta yuko tayari kuondoka Nou Camp kabla hajazungumza mambo mengine zaidi.

Pep Guardiola anaweza kujaribu na kutumia uhusiano wake na Iniesta kumfanya atue Manchester City

Alisema: ''Sijui kama ni kweli hivyo, napendelea kusubiria na kuaona uamuzi wake – atabaki Barcelona au ataondoka.

''Namtakia mafanikio mema. Ilikuwa ni furaha kwangu mimi kuwa mchezaji mwenzake na kisha kuwa meneja wake.'' 

Guardiola alikuwa mkufunzi wa Iniesta wakati alipokuwa meneja wa Barcelona kuanzia mwaka 2008 hadi 2012
Guardiola atajaribu kumshawishi kiungo huyu wa Barcelona ajiunge na Man City Guardiola atajaribu kumshawishi kiungo huyu wa Barcelona ajiunge na Man City Reviewed by Zero Degree on 4/24/2018 03:32:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.