Loading...

Inter Milan yaionya Chelsea kuelekea usajili wa majira ya joto

Inter Milan yaionya Chelsea kuelekea usajili wa majira ya joto
Inter Milan haitamuuza nyota anayewindwa na klabu ya Chelsea, Mauro Icardi kama haitafuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa, anasistiza mkurugenzi wa kandanda wa klabu hiyo, Piero Ausilio.

Hadi hivi sasa, Inter Milan iko nafasi ya tano kwenye Serie A, ikiwa nyuma ya Lazio ambayo iko nafasi ya nne kwa pointi moja tu.

Ripoti zilizotoka mwanzoni mwa mwaka huu zilidai kuwa kufuzu kushiriki michuano ijayo ya Klabu Bingwa ilikua muhimu kwa klabu hiyo ya San Siro, hivyo wanaweza kuhikikisha hilo linawezekana. Kama sivyo, iliripotiwa kuwa Inter inaweza kulazimika kuwauza wachezaji wao wa muhimu kama vile, Icardi, ambaye anawindwa na Chelsea.

Ausilio alisema: “Kama msimu ungeisha leo, tungekuwa tumeshindwa kufikia malengo yetu ya kushiriki Ligi ya Mabingwa,

“Lakini bado kuna mwanya wa pointi moja tu na michezo mitano kabla ya ligi kumalizika. Nafasi bado iko wazi.

“Tuna mipango mingi kwa wakati ujao, yote ikiwa ni pamoja na michuano ya kama tutashiriki Ligi ya Mabingwa au la.

Mauro Icardi
“Sidhani kama itatulazimu kumuuza mchezaji mkubwa kama hatutafuzu kushiriki michuano hiyo.”
Inter Milan yaionya Chelsea kuelekea usajili wa majira ya joto Inter Milan yaionya Chelsea kuelekea usajili wa majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 4/25/2018 11:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.