Kim Jong un akubali kuangamiza silaha za kinyuklia Korea
Kim Jong un na mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in |
Runinga ya serikali imemlimbikizia sifa na kumpa hongera Kim Jong-un kwa kufanikisha hayo wakisema ni kutokana na upendo wake kwa raia wake na kutaka pia nchi hiyo iweze kujitegemea .
Msimamo huo ni tofauti na jinsi vyombo vya habari vya Korea kusini walivyouchambua mkutano huo.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa swala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia, wakihoji kuwa hakutoa hakikisho lolote linaloweza kuaminika.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataendelea kuishinikiza Korea kaskazini kuachana na miradi yake ya kinyuklia licha ya mafanikio makubwa ya mkutano wa jana baina ya viongozi wa Korea ya Kusini na Kim Jong Un wa Korea kaskazini.
Trump pia amesisitiza azma yake ya kukutana na kiongozi huyo wa Korea kaskazini kwa matumaini kwamba ataweza kumshawishi asiendelee kujilimbikizia silaha hizo hatari.
Katika mkutano huo wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi Kim Jong un alikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea kusini Moon Jae-in, katika kuhakikisha hamna silaha kinyuklia katika rasi nzima ya Korea.
Hata hivyo wadadisi wa maswala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa swala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia.
Korea Kazkazini imewekewa vikwazo vya kiuchumi chungu nzima kutokana na kukataa kwake kusitisha miradi hiyo ya kinyuklia ambayo imekuwa ikiwatia wasiwasi jirani zake , Korea Kusini, Japan na washirika wao wa karibu Marekani - wanaosema inawahatarishia usalama wao.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataendelea kuishinikiza Korea kaskazini kuachana na miradi yake ya kinyuklia licha ya mafanikio makubwa ya mkutano wa jana baina ya viongozi wa Korea ya Kusini na Kim Jong Un wa Korea kaskazini.
Trump pia amesisitiza azma yake ya kukutana na kiongozi huyo wa Korea kaskazini kwa matumaini kwamba ataweza kumshawishi asiendelee kujilimbikizia silaha hizo hatari.
Katika mkutano huo wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi Kim Jong un alikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea kusini Moon Jae-in, katika kuhakikisha hamna silaha kinyuklia katika rasi nzima ya Korea.
Rais Kim Jong un |
Korea Kazkazini imewekewa vikwazo vya kiuchumi chungu nzima kutokana na kukataa kwake kusitisha miradi hiyo ya kinyuklia ambayo imekuwa ikiwatia wasiwasi jirani zake , Korea Kusini, Japan na washirika wao wa karibu Marekani - wanaosema inawahatarishia usalama wao.
Kim Jong un akubali kuangamiza silaha za kinyuklia Korea
Reviewed by Zero Degree
on
4/28/2018 11:05:00 AM
Rating: