Loading...

Mpina (ACT) apindua meza mahakamani


Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Luhaga Mpina ameshinda kesi ya kupinga kuzuiwa kurejesha fomu za uteuzi wa mgombea Urais iliyofunguliwa dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambapo Mahakama imeamuru taratibu ziendelee zilipoishia.

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Masijala ya Dodoma, ilisikiliza hoja za pande zote septemba 8,2025 na siku ya leo Mpina aliwasili Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa shauri hilo.

Mahakama imetoa uamuzi huo huku ikiweka wazi kuwa Tume huru ya uchaguzi ni chombo huru hivyo hakiwajibiki kufuata amri ya mtu yoyote au taasisi yoyote ya Kiserikali.
Mpina (ACT) apindua meza mahakamani Mpina (ACT) apindua meza mahakamani Reviewed by Zero Degree on 9/11/2025 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.