Loading...

Liverpool inatarajiwa kumsajili kiungo huyu kutoka Ureno


Emre Can anatarajiwa kuondoka Liverpool kama mchezaji huru kwenye majira ya joto, kwani mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu. Kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa katika safu ya kiungo na wekundu hao wanatafuta mbadala wake. Wamekuwa wakihusishwa na wachezaji kadhaa akiwemo na kiungo wa Napoli, Jorginho.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwandishi wa habari wa Ureno, Marcus Alves, Liverpool wanatarajiwa kumsajili kiungo wa klabu ya Wolves, Ruben Neves kwenye majira ya joto. Marcus ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa twitter.

Ruben Neves 
Ruben ametoa mchango mkubwa sana kwa Wolves msimu huu. Amefunga magoli 6 na kutoa assist 1 akicheza katika nafasi ya kiungo mkabaji, kitu ambacho ni kizuri sana na anajulikana kwa kufunga magoli ya kushangaza. 

Mreno huyo alijiunga na Wolves akitokea Porto kwenye majira ya joto mwaka jana kwa pauni milioni 16 na kwa mujibu wa Marcus, Wolves wanamtegemea nyota anayeichezea Besiktas kwa mkopo kutoka Benifica, Anderson Talisca achukue nafasi yake kama Mreno huyo ataamua kuondoka.

Manchester United pia wanamtamani Ruben na ripoti zinadai kuwa mashetani hao wamemchunguza mara kadhaa msimu huu.

Ingawa klabu ya Wolves imesema inafurahia huduma ya Ruben na kuwa haina mpango wa kumuuza inaonyesha kuwa 
itakuwa ni kazi ngumu kwa Liverpool kumsajili kiungo huyo kutoka klabu ambayo inapanda daraja kwenda kucheza Ligi Kuu ya Uingereza, .
Liverpool inatarajiwa kumsajili kiungo huyu kutoka Ureno Liverpool inatarajiwa kumsajili kiungo huyu kutoka Ureno Reviewed by Zero Degree on 4/19/2018 08:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.