Loading...

Manchester United inaweza kuambulia patupu kwa beki huyu

Mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho
Tangu ajiunge na Barcelona, Samuel Umtiti amekuwa nguzo katika safu yao ya ulinzi. Akionyesha uwezo mkubwa akiwa na klabu hiyo na sasa ameingia kwenye orodha ya mabeki bora wa dunia.

Uwezo wake umezivutia klabu nyingi barani Ulaya na thamani na thamani yake kwa sasa ikiwa karibu sawa na puni milioni 53, itakuwa ni rahisi sana kwa klabu hizo kumnasa beki huyo.

Barcelona wanalitambua hilo na tayari wana mpango wa kuanza mazungumzo ya kandarasi mpya na raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. Lakini mchezaji huyo bado anasumbua kufanya maamuzi kwani anataka aongezewe mshahara, kitu ambacho kimekwamisha mazungumzo kati yao.

Manchester United wako tayari kuitumia nafasi hiyo, huku Jose Mourinho akiwa ametoa kipaumbele kwa safu ya ulinzi kwenye usajili wa majira ya joto. Mreno huyo ni shabiki mkubwa wa beki huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa na amemjumuisha kwenye orodha ya wachezaji anaowahitaji.

Lakini, kwa mujibu wa taarifa ya Mundo Deportivo, vigogo hao wa La Liga wanashauku kubwa ya kufikia makubaliano na watampa beki huyo ofa mpya yenye maslahi mazuri ili kumshawishi asalie Nou Camp. Na sehemu ya dili hili litaambatana na ongezeko la thamani yake hadi karibu sawa na pauni milioni 220.

Wanapanga kumpa ofa kubwa itakayoambatana na ongezeko kubwa kwenye mshahara wake wa sasa, kitu ambacho kinawapa matumaini kwamba atakubali kusaini mkataba huo kabla ya Kombe la Dunia mwezi June.

Beki wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Ufaransa, Samuel Umtiti
Kama Mfaransa huyo atasaini mkataba mpya, hivyo itakuwa ni pigo kubwa kwa Manchester United na wanaweza kulazimika kuelekeza nguvu zao kwingine.
Manchester United inaweza kuambulia patupu kwa beki huyu Manchester United inaweza kuambulia patupu kwa beki huyu Reviewed by Zero Degree on 4/20/2018 08:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.