Loading...

Sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani - Kheri James

Kheri James
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Taifa UVCCM, Kheri James amesema haitoweza kuja kutokea Chama cha Mapinduzi 'CCM' kutolewa madarakani katika chaguzi zozote zile kwa madai watanzania wa sasa wanaakili sana katika kuamua mambo yao hasa kwenye uchaguzi.

Kheri ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali la miongoni mwa mashabiki zake waliotaka kufahamu kwamba je itakuja kutokea siku chama cha Mapinduzi kitashindwa kushinda katika uchaguzi mkuu na upinzani kuchukua madaraka.

"Kwa kipindi hiki ambacho watanzania wana akili timamu sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani. Watanzania wana akili sana na wanaiona kesho kubwa ya nchi hii na usalama wa Tanzania bado upo kwenye chama cha Mapinduzi. Hatuzui wapinzani lakini kwa dola ni CCM tu itaendelea kutawala sana", amesema Kheri.

Kwa uapande mwingine, Kheri amesema kumekuwepo na wanasiasa wengi wanaingia kwenye uwanja huo kwa kufuata mkumbo na kuacha misingi ya kisiasa ambayo ni kuzungumza kwa hoja zilizokuwa na tija kwa jamii pamoja na taifa.
Sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani - Kheri James Sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani - Kheri James Reviewed by Zero Degree on 4/05/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.