Loading...

Singida United yaikomalia Yanga SC


Klabu ya soka ya Singida United imeendeleza rekodi yake ya kutofungwa na mabingwa wa soka nchini Yanga kwenye mechi walizokutana tangu msimu huu uanze baada ya leo kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi kuu.

Katika mchezo huo uliomalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Singida United ndio ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya pili tu kipindi cha kwanza kupita kwa nyota wake wa kimataifa raia wa DR Congo Kambale Salita 'Papy'.

Yanga ilibidi wasubiri dakika za mwisho kipindi cha kwanza ndipo wakasawazisha bao kupitia kwa mlinzi wake wa kati Abdallah Shaibu maarufu kama Ninja baada ya kumalizia kwa kichwa kona iliyopigwa na Ibrahim Ajib.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Yanga kufikisha alama 47 kwenye michezo 22 ikiwa nyuma kwa alama 5 mbele ya vinara wa ligi Simba SC wenye alama 52 katika mechi 22. Singida United imefikisha alama 37 ikiendelea kusalia katika nafasi ya tano baada ya michezo 23.

Kesho vinara wa ligi hiyo Simba SC watashuka kwenye uwanja wa taifa kuwakaribisha Mbeya City kwenye mchezo wao wa raundi ya 23 huku Azam FC wakiwa ugenini kucheza na Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Singida United yaikomalia Yanga SC Singida United yaikomalia Yanga SC Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.