Straika Manchester United ashauriwa kutimkia Arsenal, Chelsea au Liverpool
Rashford ‘anaweza akaondoka Manchester United msimu ujao’ kama ataendelea kuanzia benchi.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza ameambiwa na aliyekuwa nyota wa Newcastle, Micky Quinn aondoke Manchester United akatafute muda wa kutosha dimbani.
Inaonekana nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 alichukizwa na kitendo cha kuanzia benchi kwenye mechi ya Man United dhidi ya City wikendi iliyopita.
Rashford ameanza na kikosi cha kwanza kwenye michezo mitano kati ya 16 ya mwisho na inasemekana alichukizwa zaidi na jambo la kuanzia benchi katika mechi ya mahasimu wao wakubwa Jumamosi, iliyomalizika kwa United kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester City.
Hata hivyo, Rashford anafurahia msimu wake wa magoli akiwa na jezi ya United, akiwa ameshafunga magoli 12 hadi hivi sasa.
Marcus Rashford |
Akimzungumzia Rashford, Quinn alisema: “Nafikiri anatakiwa kuondoka. Sio chaguo la kwanza la Jose Mourinho.
“Kijana huyo ni mmoja kati ya wachezaji wenye uwezo mkubwa tuliowahi kuwaona wakiwa na jezi ya Manchester United – inanibidi niseme hivyo.
“Kama anataka muda wa kutosha uwanjani, sidhani kama ataupata kwa Jose Mourinho. Lukaku ndio chaguo la kwanza uwanjani.”
Straika Manchester United ashauriwa kutimkia Arsenal, Chelsea au Liverpool
Reviewed by Zero Degree
on
4/10/2018 02:25:00 PM
Rating: