Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 12 Aprili, 2018
Robert Lewandowski |
PSG inatarajiwa kuongeza juhudi katika kuwania saini ya mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, huku ikiaminiwa kuwa raia huyo wa Scotland amemwambia wakala wake amtafutie timu mpya. (L'Equipe)
Hamburg inaweza kumpoteza nyota anayewindwa na klabu ya Tottenham, Jan-Fiete Arp, ambaye anaweza kwenda Bayern Munich kama klabu hiyo itashuka daraja mismu huu. (Bild)
Marcus Rashford anafurahia kuishi ndoto zake kwa kuichezea klabu yake ya nyumbani licha ya kukosa muda wa kutosha katika kikosi cha kwanza cha United.
Gareth Bale anaedndelea kuhusishwa na uhamisho kwenda Manchester United, lakini taarifa zinadai kuwa raia huyo wa Wales sio chaguo la kwanza la Jose Mourinho. (Manchester Evening News)
Franck Ribery amesaini mkataba mpya na Bayern Munich, ambao utamfanya aendelee kuitumikia klabu hiyo hadi kwenye majira ya joto 2019. (Kicker)
Alex Oxlade-Chamberlain anasema kuwa Liverpool haihofii kupangwa na timu yoyote kwenye Ligi ya Mabingwa.
Chelsea ilikosea kumruhusu Diego Costa aondoke Stamford Bridge, kwa mujibu wa Avram Grant.
Cristiano Ronaldo anasema uamuzi wa mwamuzi Michael Oliver kutoa penalti ulikuwa sahihi na anawashangaa Juventus kulalamikia jambo hilo.
Arsene Wengere amesama kuwa lengo la kuu la klabu ya Arsenal kwa sasa ni kutwaa taji la Ligi ya Europa.
Giuliano Terraneo |
Klabu ya West Brom imemteua mkurugenzi wa kandanda kutoka Italia, Giuliano Terraneo kuwa mshauri wao kwenye benchi la ufundi. (Sky Sports)
Arsenal wanajiandaa kumsajili kiungo wa Atletico Madrid, Saul Niguez, ambaye mkataba wake utamruhusu kuondoka kwa pauni milioni 130.
Manchester United ilimchunguza beki wa Swansea, Alfie Mawson kwenye mechi wao dhidi ya West Brom uliomalizika kwa timu hizo mbili kutoka sare ya goli 1-1 wikendi iliyopita
Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola anatafakari uwezekano wa kurejea sokoni kusaja saini ya Riyad Mahrez, Leon Bailey na Thomas Lemar kwenye majira ya joto. (Sun)
Manchester United wako tayari kuigalagaza Chelsea kwa kutoa ofa ya pauni milioni 40 kwa ajili ya winga wa klabu ya Watford, Richarlison.
Pep Guardiola atasaini mkataba mpya na klabu ya Manchester City kabla msimu huu haujaisha.
Meneja wa West Ham, David Moyes ana ujasiri wa kumnasa beki wa klabu ya Fulham, Ryan Fredericks.
Millwall wanahofia kushindwa kumsajili winga wa klabu ya Wolves, Ben Marshall kwa mkataba wa kudumu kwenye majira ya joto kutokana na bei kubwa.
Michael Dawson |
Hull City inakabiliana na ushindani mkubwa kumbakisha beki wao, Michael Dawson, ambaye anawindwa na klabu ya Nottingham Forest. (Mirror)
Pep Guardiola anakabiliwa na adhabu ya kukosa mechi tatu za Ligi ya Mabingwa baada ya kutuhumiwa kwa makosa mawili tofauti. (Times)
Jose Mourinho ameshamwambia Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Manchester United, Ed Woodward kuhusu wachezaji watatu anaowahitaji kwenye majira ya joto. (Express)
Pep Guardiola anaweza kutumia kiasi cha pauni milioni 600 katika klabu ya Manchester City kwa usajili wa wachezaji watatu wenye majina makubwa kwenye majira ya joto - kiungo mkabaji, mshambuliaji hodari na beki wa kati wakiwa vinara kwenye orodha yake.
Muda wa Jese Rodriguez katika klabu ya Stoke City unaweza kuwa umefikia kikomo baada ya nyota huyo kushindwa kufika katika mazoezi ya timu hiyo Jumatano. (Telegraph)
Chelsea imejiunga na Manchester United pamoja na Manchester City kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri.
Danny Drinkwater anafikiria juu ya hatima yake katika klabu ya Chelsea baada ya kutumia muda mwingi akiwa amekaa benchi kwenye msimu wake wa kwanza Stamford Bridge.
Manchester City ina mpango wa kumsajli beki wa klabu ya Sao Paulo, Eder Militao anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 20. (Daily Mail)
David Luiz |
David Luiz ameanza kufanya mazoezi katika klabu ya Chelsea, akijaribu kurejea kwenye hali yake ya kawaida kutoka kuuguza majeraha ya goti na kifundo cha mguu na ajaribu kulinda nafasi yake kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 12 Aprili, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2018 11:15:00 AM
Rating: