Loading...

Shule ya Sekondari Lindi yateketea kwa moto.

Shule ya Sekondari Lindi ya inayomilikiwa na Serikali imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo, chanzo kikidaiwa ni hitilafu ya umeme.

Katika tukio hilo vyumba tisa vya madarasa, ofisi nne za walimu na samani zake, vyoo na sehemu ya maabara za fizikia na baiolojia ziliteketea.



Mkazi wa mtaa wa Rahaleo ilipo shule hiyo, Mohamedi Bakari amesema kuwa walipata taarifa ya moto saa 6.30 usiku na walipofika eneo la tukio walikuta moto umeanza kuwaka na baada ya muda lilifika gari la zimamoto lakini halikufanya kazi kwa madai kuwa bomba la kutoa maji ni mbovu.


Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renata.

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Renata Mzinga amesema moto huo ulioanza saa saba usiku ulitokana na hitilafu ya umeme kwa kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa ulianzia kwenye main switch na kusambaa.

Mzinga aliongeza kuwa kwenye tukio hilo alikamatwa mtu mmoja ambaye alitumia fursa hiyo kuiba kompyuta mpakato ambayo iliokolewa kwenye moja ya ofisi za shule hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi ametoa shukrani kwa wananchi walivyoshiriki kusaidia kuokoa mali.





ZeroDegree.
Shule ya Sekondari Lindi yateketea kwa moto. Shule ya Sekondari Lindi yateketea kwa moto. Reviewed by Zero Degree on 7/10/2016 01:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.