Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Aprili, 2018

Jerome Boateng
Manchester United inapanga kujaribu kumsajili beki wa klabu ya Bayern Munich, Jerome Boateng.

Antoine Griezmann amesema kuwa ataamua juu ya hatima yake baada y kufanya mazungumzo na klabu ya Atletico Madrid.

Zinedine Zidane amesema kuwa atafanya lolote liwezekanalo kuwashawishi Gareth Bale na Karim Benzema kuwa ni wachezaji muhimu kwao.

Unai Emry amethibitisha kuwa ataondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu.

Antonio Conte anasistiza kuwa haitakuwa uungwana kuikosoa Chelsea kwa kumuuza Salah kwenda Roma kwa sababu raia huyo wa Misri amekuwa mtu mpya kwa sasa.
 
Aliyekuwa kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard anatarajia kufanya mazungumzo zaidi na klabu ya Rangers . (ESPN)
 
Diego Maradona amejiuzulu kazi ya kuinoa klabu ya Al Fujairah kutoka Falme za Kiarabu baada ya klabu hiyo kushindwa kupanda daraja.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa bado wanaendelea na mapambano ya kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Sky Sports)

Diego Simeone
Meneja wa Atletico Madrid, Diego Simeone atazuiliwa kufanya mawasiliano ya aina yoyote na wachezaji wake kwenye mechi ya pili ya nusu fainali ya Europa Ligi dhidi ya Arsenal.

West Brom wako tayari kujaribu kumshawishi meneja wa klabu ya Bristol City, Lee Johnson kuwa mkufunzi wao mpya.

Vigogo wa Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA) wameshindwa kupata mdhamini mpya kuelekea michuano ya Kombe la Dunia. (Sun)

Arsene Wenger anaweza kuwa meneja anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kama ataenda China.

Antonio Conte atamchezesha Gary Cahill kwa muda wote uliosalia msimu huu kumpa matumaini ya kushiriki Kombe la Dunia.

Kiungo wa Stoke City na timu ya taifa ya Senegal, Badou Ndiaye anafuatiliwa na klabu za Uturuki Besiktas pamoja na Galatasaray. (Mirror)

Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez amesema kuwa yuko kwenye mazungumzo ya kusaini mkataba mpya kuelekea mchezo wao dhidi ya West Brom.

Barcelona na Manchester United wako makini baada ya mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann kusema kuwa hajui atakua wapi msimu ujao. (Express)

Uwanja wa Wembley
Wanachama wa bodi ya FA walikabiliwa na tukio la wadau kuwapigia kura ya kutokuwa na imani siku ya Ijumaa juu ya mpango wao wa kuuza Uwanja wa Wembley.

Bournemouth na Brighton zinatafakari juu ya kujaribu kumsajili nyota wa klabu ya Hibernian, John McGinn anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 3.

David Moyes amekuwa akiwafundisha wachezaji wake wa West Ham namna ya kucheza bila mpira kwa sababu anatambua kuwa Manchester City watautawala mpira siku ya Jumapili. (Daily Mail)

Nafasi ya Antonio Conte kurejea kuwa meneja wa timu ya taifa ya Italia imepotea kufuatia Muitaliano huyo kudaia mkataba wa miaka mitano.

James Milner ameikataa nafasi ya kurejea katika timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia baada maoni yake kwa FA. (Times)

Rangers inaendelea kuwa na ujarisi wa kumteua Steven Gerrard kuwa meneja wao mpya lakini uamuzi unategemeana na kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool. (Guardian)

Meneja wa Stoke City, Paul Lambert anasema kuwa Liverpool itakuwa kwenye hatari kubwa kumchezesha Mo Salah dhidi yao kuelekea mchezo wao na Roma kwenye Ligi ya Mabingwa.

PSG watamuuza Neymar endapo tu watakutwa na hatia ya kukiuka kanuni za usajili.

Arsene Wenger
Arsene Wenger amekumbushia ofa aliyopewa ya ya kuwa meneja wa klabu ya Manchester United, lakini anasistiza kwamba alikuwa mzalendo kwa Arsenal siku zote. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 28 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/28/2018 10:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.