Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Aprili, 2018

Andrea Belloti
Rais wa Torino, Urbano Cairo amesema kuwa nyota wa klabu hiyo anayewindwa na Chelsea, Andrea Belloti anaweza kuhamia Uhispania au Uingereza, lakini ni kama tu klabu inayomhitaji italipia kiasi cha pauni milioni 87. (Tuttosport)

Nyota anayewaniwa na Manchester City, Andres Iniesta ameripotiwa kuwa nia ya kuhamia China kwa mwaka mzima uliopita, lakini anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza kwa Mabingwa hao wa EPL au Arsenal. (AS)

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anabakia kuwa na imani na mshambuliaji wa klabu hiyo, Karim Benzema. (Marca)

Patrick Vieira amesema kuwa hajawasiliana na mtu yoyote kutoka Arsenal juu ya kuchukua nafasi ya Arsene Wenger kama meneja mpya wa klabu hiyo.

Aliyekuwa nahodha wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrard anasema kuwa Mohamed Salah ni mchezaji bora wa Dunia. (ESPN)

Ralf Rangnick yuko kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal.

Nahodha wa Aston Villa, John Terry amesema kuwa bado "ana njaa" ya kucheza soka na ataamua juu ya hatima yake katika klabu hiyo kwenye majira ya joto.
 
Partrick Vieira anasema kuwa atakuwa tayari kuinoa klabu ya Arsenal kama atapokea wito kutoka kwao.

Gareth Bale
Gareth Bale anasema kuwa anahisi kuheshimiwa kwa kuhusishwa na uhamisho kwenda klabu ya Bayern Munich.

Allan Mcgregor anakaribia kusaini mkataba wa awali wa makubaliano ya kurejea katika klabu ya Rangers. (Sky Sports)

Manchester United watalazimika kumtoa Luke Shaw pamoja na ofa ya pauni milioni 40 kama wanataka kumsajili beki wa Tottenham, Danny Rose kwenye majira ya joto.

Aliyekuwa rais wa Real Madrid, Ramon Calderon anasema kuwa klabu hiyo itamsajili mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski kwa lengo la kusogeza muda kumsubiria Harry Kane.

Hector Bellerin ameashiria kwamba ana mpango wa kubaki Arsenal - kwa kusema kuwa anataka jezi namba 2. (Sun)

Arsenal wanaamini wanaiongoza Chelsea kwenye mbio za kuwania kumfanya Luis Enrique kuwa meneja wao mpya lakini wanaweza kukwamishwa na suala la mshahara wa pauni milioni 15 kwa msimu.

RB Leipzig wanawania kumsajili chipukizi wa Tottenham, Reo Griffiths, ambaye amefunga zaidi ya magoli 30 akiwa na timu ya vijana na klabu hiyo msimu huu.

Mashabiki wa Chelsea na Manchester United wanaungana pamoja kuomboleza kifo cha Ray Wilkins, ambaye alikutwa na umauti mapema mwezi huu, wakati watakapokutana kwenye fainali ya FA Cup tarehe 19 mwezi Mei.

Lucas Halter
Pep Guardiola anamchunguza beki chipukizi wa timu ya taifa ya Brazil U20, Lucas Halter, ambaye anaichezea klabu ya Atletico Paranaense, kuongeza uhusiano wake na Amerika ya Kusini katika klabu ya Manchester City.

Robin van Persie ameashiria kuwa anakaribia kustaafu, huku akikiri kwamba lazima awe 'mwaminifu' kwa nafsi yake.

Jamaal Lascelles anadai kuwa Newcastle imeziba midomo ya wale walioibeza timu yao.

Carlo Ancelotti anatarajiwa kuwa meneja mpya wa timu ya taifa ya Italia lakini tu kwa sababu ametoshwa na Arsenal pamoja na Chelsea.

Manchester City wamejiondoa kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Shakhtar Donetsk, Fred na kuisafishia njia Manchester United. (Star)

Chelsea haitakubali ofa kwa ajili ya Tiemoue Bakayoko na Alvaro Morata kwenye majira ya joto isipokuwa kama wachezaji hao wataweka wazi kuwa wanataka kuondoka. 
(Telegraph)

Allan McGregor anakaribia kurejea katika klabu ya Rangers.

Cristiano Ronaldo aliendeleza mkakati wake wa kutoa zawadi kwa kumtumia mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford jezi ya Real Madrid iliyosainiwa. (Daily Mail)

Joachim Low
Joachim Low anasita kuchukua nafasi ya Arsene Wenger kama meneja mpya wa Arsenal kwenye majira ya joto. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 25 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/25/2018 10:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.