Loading...

Chadema wakana maandamano ya Aprili 26


Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja, Idrissa Jumbe Mkila, amesema chama hicho hakihusiki na maandamano yoyote yanayotarajiwa kufanyika kesho.
Mkila ameyasema hayo leo Aprili 25 wakati akizungumza na waaandishi wa habari katika ufunguzi wa mafunzo maalum ya kuwajengea uwezo viongozi wa chama Wilaya na Mikoa huko Kikwajuni Mkoa Mjini Unguja.

“Hatuna taarifa na hatuna nafasi ya kujiingiza katika mambo kama hayo ambayo hayana tija kwa mustakabali wa kujenga nchi,” amesema.

Ameongeza: “Kama chama tumeshatoa maelekezo kwa viongozi wetu na wanachama wetu kutoshiriki maandamano na tunawaomba wanachama waendelee na shughuli zao za kila siku za maisha kwa sababu leo ni siku adhimu ya kumbukumbu ya Muungano wetu.” 

Akizungumzia maandamano hayo, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohamed Haji Hassan amesema kuwa vikosi vyake vyote vya ulinzi vipo vizuri na kuongeza kuwa yeyote atakayethubutu kushiriki maandamano hayo atachukuliwa hatua.

Source: Mwananchi
Chadema wakana maandamano ya Aprili 26 Chadema wakana maandamano ya Aprili 26 Reviewed by Zero Degree on 4/25/2018 10:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.