Loading...

Ukuta wa Tanzanite waingiza zaidi ya milioni 700


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu, serikali imepata mapato ya Sh milioni 714 ikilinganishwa na Sh milioni 147.1 zilizopatikana kwa mwaka wote wa mwaka 2017.

Amesema hali hiyo inatokana na hatua zilizochukuliwa baada ya kuimarisha ulinzi wakati wa ujenzi wa ukuta kwenye migodi ya Tanzanite, huko Mirerani mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Ofisi yake, kwa mwaka 2018/19, Majaliwa amesema; “mapato hayo yameongezeka tu baada ya kuimarisha ulinzi wakati wa ujenzi wa huo ukuta.”

Amesema mbali na manufaa hayo, pia katika eneo hilo la Mirerani zitajengwa nyumba za kuuzia madini hayo jambo litakalokuwa na manufaa kwa wananchi wa eneo hilo pia.
Ukuta wa Tanzanite waingiza zaidi ya milioni 700 Ukuta wa Tanzanite waingiza zaidi ya milioni 700 Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 06:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.