Ummy asisitiza wanaume kupima tezi dume
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) na Naibu Waziri wa wizara hiyoDkt. Faustine Ndugulile |
Ameyasema hayo wakati akizindua kampeni ya chanjo ya saratani ya kizazi na uchunguzi wa saratani ya kizazi kwa wanawake iliyofanyika kituo cha Afya cha Ngamiani, Jumamosi. Amesema tatizo la saratani kwa wanawake na wanaume katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, ikiwemo Tanzania linaongezeka kila mwaka hivyo ni vema kuwakachukua tahadhari. Kwa wanawake, amesema takwimu za taasisi ya uchunguzi wa saratani nchini ya Ocean Road kila wagonjwa 100 wa saratani, 45 kati yao ni wanawake wenye saratani ya kizazi na matiti.
“Nataka niwaambie Watanzania kuwa saratani ikigundulika mapema inazuilika na kinga ni bora kuliko tiba…juzi nilikutana na viongozi wa dini ya kiislamu Dar es Salaam wakaniambia kuna aya kwenye Kurani inasema chukueni tahadhari kwenye afya zenu, hivyo wanaume msiogope kipimo cha saratani ya tezi dume hata nyinyi pia mnatakiwa kufanyiwa uchunguzi, nendeni vituo vya afya na hospitali mkapimwe msiwaachie wanawake peke yao,” alisema.
Waziri amewashauri madaktari katika vituo vya afya wanapowafanyia uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi wanawake na wakabainika na dalili wasifanye haraka ya kuwapa tiba ya kukandamiza (cryotherapy) badala yake wawape nafasi kushauriana na wenza wao ili kuepusha mgogoro ya ndoa.
Ummy asisitiza wanaume kupima tezi dume
Reviewed by Zero Degree
on
4/30/2018 04:49:00 PM
Rating: