Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kiungo huyu kutoka Serie A
Kiungo wa klabu ya Atalanta, Bryan Cristante |
Soma na hizi:
Ntota huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) baada ya Atalanta kukamilisha vigezo vya kumsajili kwa mkataba wa kudumu toka usajili wa mkopo kutoka Benfica mapema mwaka huu.
Inaeleweka kuwa mawakala wa Cristante walikutana na vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza mjini London wiki mbili zilizopita na kwa upande wake mchezaji huyo anaonekana kuwa na hamu ya kutua Uingereza. Hata hivyo, taarifa hiyo inadaia kwamba Muitaliano huyo mwenye asili ya Canada pia anawindwa na vilabu vikubwa kutoka Italia na Ujerumani.
Soma na hizii:
Soma na hizii:
- Abramovich achagua mchezaji anayemtaka awe nahodha wa Chelsea
- Sababu ya Conte kutaka kuondoka Chelsea yabainika
Cristante alionekana kwenye kikosi cha kwanza cha AC Milan kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na umri wa miaka 16, baadaye alinunuliwa na Benfica kwa karibu pauni milioni 5 mwaka 2014 lakini alifanikiwa kuichezea klabu hiyo michezo sita pekee ya Ligi Kuu ya Ureno, kutuzitumikia Palermo na Pescara za Italia kwa mkopo.
Ameibuka na kuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha uwezo wa kuvutia msimu huu, akifunga magoli 12 katika michezo 44, na kupata nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza mwezi Octoba.
Ameibuka na kuwa miongoni mwa wachezaji walioonyesha uwezo wa kuvutia msimu huu, akifunga magoli 12 katika michezo 44, na kupata nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa kwa mara ya kwanza mwezi Octoba.
Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kiungo huyu kutoka Serie A
Reviewed by Zero Degree
on
4/30/2018 04:49:00 PM
Rating: