Loading...

Abramovich achagua mchezaji anayemtaka awe nahodha wa Chelsea

Mimiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovic
Ian McGarry anadai kwamba, mmiliki wa klabu ya Chelsea anataka David Luiz awe nahodha wa timu hiyo, sio Gary Cahill.

Anasema kuwa beki huyo anapendwa sana na Abramovich, ambaye alitaka Luiz arithi nafasi ya John Terry.

Beki wa klabu ya Chelsea, David Luiz
Antonio Conte alimwacha David Luiz nje kwenye kikosi kilichocheza mechi ya mwisho, ambayo ilimalizika kwa Chelsea kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United.

Na McGarry anasema kwamba, 
kwa kitendo hicho alichokifanya meneja wa Chelsea ni sawa na kumchokonoa bosi wake.

“David Luiz alirudishwa kikosini Chelsea kwa sababu ni mmoja wa wachezaji wanaopendwa na Roman Abramovich,” alisema McGarry.


“Hakuwa chaguo la mtu yeyote kwenye benchi la ufundi la klabu ya Chelsea.

“Anapendwa na mmiliki wa klabu, ambaye alimchukua aje kumrithi John Terry kama nahodha wa klabu, na ukweli ni kwamba Gary Cahill kuendelea kuwa nahodha badala ya Luiz linabaki ni suala ambalo Roman Abramovich anapingana nalo kila kukicha.

“Kwa kitendo cha kumwacha nje ya kikosi, ilikuwa ni kumchokonoa Roman Abramovich .”
Abramovich achagua mchezaji anayemtaka awe nahodha wa Chelsea Abramovich achagua mchezaji anayemtaka awe nahodha wa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 11/14/2017 05:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.