Loading...

Takukuru yaahidi kutoa dau la milioni 10 kwa atakayempata mhasibu aliyetoroka

Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) yaahidi kutoa milioni 10 kwa mtu yeyeote atakayetoa taarifa mahali alipo aliyekuwa mtumishi wa taasisi hiyio Bwana Godfrey John Gugai ambaye wanamtafuta kwa kuwa na mali nyingi kinyume na sheria.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo Naibu Mkurugenzi wa TAKUKURU,  Brigedia Jenerali John Mbungo amesema mtu huyo awali alianza kuonyesha ushirikiano walipoanza kumuhoji, lakini baada ya muda akaanza kuwakwepa na hatimaye kutokomea kusikojulikana.

"Tumeendelea kumtafuta na taarifa tulizozipata amekuwa anakimbia nchi kupitia njia ambazo sio rasmi na hadi sasa tumeendelea kumtafuta lakini bado hajapatikana. Na sisi tumeona ni vema tuziweke hizi habari ziwe wazi kwenu waandishi wa habari na wananchi, popote watakapompata au kumuona huyu bwana watoe taarifa katika chombo hiki na taasisi hiii itamzawadia mtu yeyote ambaye atafanikisha kupatikana kwa huyu mtu, zawadi ya milioni 10 pesa taslim.", amesema Brigedia Mbungo.

Godfrey Gugai alikuwa mhasibu wa TAKUKURU anatuhumiwa kuwa na mali nyingi kinyume na sheria kwa mtumishi wa umma, ambapo ana nyumba ya ghorofa 4 iliyopo Ununio Knondoni, nyumba ya ghorofa 3 Bunju, ana nyumba za kupangishwa Mbweni, ana nyumba za kupangisha Kinondoni, ana jengo la kifahari Majita Musoma, ana nyumba Mwanza, ana nyumba ya kifahari Mwanza Nyegezi, ana viwanja lukuki sehemu mbali mbali na mali nyinginezo.
Takukuru yaahidi kutoa dau la milioni 10 kwa atakayempata mhasibu aliyetoroka Takukuru yaahidi kutoa dau la milioni 10 kwa atakayempata mhasibu aliyetoroka Reviewed by Zero Degree on 11/14/2017 04:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.