Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 14 Novemba, 2017

Paul Pogba
Paul Pogba anakaribia kurejea kikosini Manchester United lakini hategemewi kucheza dhidi ya Newcastle siku ya Jumamosi.

Rangers wanamwinda meneja wa Northern Ireland Michael O'Neill, 48, ambaye pia anatafuwa na Scotland. (Telegraph)

Klabu ya Atletico Madrid imefanya mawasiliano na nyota wa Arsenal, Mesut Ozil kuhusu kurejea Uhspania mwakani akiwa kama mchezaji huru.

Sunderland wana matumaini ya kumpata meneja wa klabu ya Barnsley, Paul Heckingbottom kama meneja wao mpya wikendi ijayo.(Sun)

West Brom wanafanya mpango wa kumsajili kiungo wa Trabzonspor, Okay Yokuslu mwezi Januari.

Javier Mascherano
Klabu ya Liverpool iko mstari wa mbele kumsajili kiungo wa Barcelona, Javier Mascherano mwezi Januari.

Aliyekuwa mchezaji wa Tottenham na Southampton Bale anaweza kurejea Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa atafurahia kufanya hivyo. (Mirror)

Arsenal wanakaribia kukamilsha dili ya kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Nabil Fekir kwa pauni milioni 60 ambaye kuwasili kwake kutafufua kuondoka kwa Mesut Ozil, 29 na Alexis Sanchez, 28.

Mshambualiaji wa Atletico Antoine Griezmann amesema kuwa ana nia ya kuhamia Paris St-Germain. Anasema kuwa kucheza klabu moja na Neymar na pia Kylian Mbappe itakuwa ndoto. (Telefoot)

Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Argentina, Enzo Diaz, ambaye anaichezea Agropecuario inayoshiriki Ligi daraja la pili.

Gianluigi Buffon amethibitisha kustaafu kucheza soka la kimataifa baada ya Italia kupoteza mchezo wao dhidi ya Sweden kwenye mtoano wa Kombe la Dunia.

Breel Embolo
Manchester City wemeingia kwenye orodha ya klabu nyingi zinazowania saini ya mshambuliaji wa Schalke 04, Breel Embolo. (Daily Mail)

Real Madrid wameamua kumuuza mshambuliaji wa Wales, Gareth Bale, 28, mwishoni mwa msimu. (AS)

Borussia Dortmund wana naia ya kumsaini mchezaji wa Liverpool Emre Can, huku mkataba wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 23 ukitarajiwa kukamilika mwishoni wa msimu. (Times)

Mshambuliaji wa Bolton Wanderers Gary Madine, 27, anataka mshambuliaji mwenzake Adam Armstrong, 20, kubaki klabu hiyo kwa mkopo kutoka Newcastle United. (Bolton News)

QPR watafungua meza ya mazungumzo juu ya mkataba wa Nedum Onuoha mwezi Januari kuepuka kumpoteza beki huyo kama mchezaji huru katika majira ya joto mwakani.

Chris Coleman
Meneja wa Wales, Chris Coleman, 47, ataihama timu ya taifa ikiwa chama cha kandanda cha wales, hakitawapa wafanyakazi wenzake mikataba ya kudumu.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte atakaribishwa kwa mikono miwili Italia akitaka kurejea, kwa mujibu wa Alessandro Del Piero. (Star)

Mshambuliaji wa Leicester City Mnigeria Ahmed Musa, 25, huende akahamia Hull City mwezi Januari. (sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 14 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 14 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/14/2017 02:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.