Loading...

Utabiri wa Hamis Kiiza, Simba Vs Yanga


Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Hamis Kiiza, ametoa utabiri wake kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Aprili 29 2018.

Kiiza ameeleza mechi hiyo itakuwa ngumu kutokana na namna asili ya timu hizo ilivyo kwa kusema yeyote atakayejipanga vizuri atapata matokeo.

Mchezaji huyo aliyeweza kung'ara wakati anazichezea klabu hizo kongwe za Kariakoo, ameweka utabiri wa asilimia 50 kwa 50 akidai mara nyingi mtanange huo huwa hautabiriki.

Kiiza hivi sasa yuko zake Ethiopia akisakata kabumbu baada ya kutoka Tanzania na baadaye kutimkia Uganda, kabla ya kuelekea Ethiopia.

Simba itakuwa mwenyeji wa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Taifa, ambapo katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi, timu hizo zilenda sare ya 1-1.
Utabiri wa Hamis Kiiza, Simba Vs Yanga Utabiri wa Hamis Kiiza, Simba Vs Yanga Reviewed by Zero Degree on 4/19/2018 04:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.