Loading...

Dkt. Bashiru arithi mikoba ya Kinana CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally mara baada ya kumpendekeza na kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam
Dkt. Bashiru Ally amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana.

Dkt. Bashiru amepitishwa leo Mei 29, 2018 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama(NEC).

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Bashiru Ally akiwa meza kuu mara baada ya kupitishwa na wajumbe wote waliohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa NEC Ikulu jijini Dar es Salaam
Dkt. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli.

Dkt. Bashiru arithi mikoba ya Kinana CCM Dkt. Bashiru arithi mikoba ya Kinana CCM Reviewed by Zero Degree on 5/29/2018 06:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.