Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 01


MTUNZI: MC Short Charles Gwimo


Haikuwa kawaida yangu kuamuka kwa kuchelewa namna hii kama nilivyochelewa leo hii. Kuamka kwa kuchelewa kulisababishwa na mihangaiko ya mwisho wa wiki iliyoambatana na mshikamano usio rasmi na kimwana Lulu ndani ya kiwanja cha fundi seramala che vipimo vya sita kwa sita. Hakika nilikua nimechoka kama vile mtu aliyekuwa akichezeshwa mahepe usiku mzima. Niliamka taratibu bila kumwamsha Lulu aliyekuwa fofofo kwa wingi wa kilevi kichwani na harakati za kuivunja amri halali ya Mwenyezi Mungu ambayo binadamu kwa viburi vyetu tunaichukulia kama ni uonevu wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake. Hizi ni kufuru kwa baadhi ya binadamu kwa mola wetu mtukufu nami nikiwa miongoni mwao.

********

Historia ya maisha yangu haipishani mbali sana kimalezi na malezi ya watoto wengi wa kiafrika hasa la kabila langu la “WAHA”. Nilizaliwa katika familia za baba mwenye ndoa za mitara ambaye alikuwa akitupenda sisi watoto wake kama kitu chenye thamani kilichopo mikononi mwa mtu. Makuzi yangu na baadhi ya ndugu zangu yalikuwa ni ya upendo wa kufunzwa kimaadili, jambo ambalo katika zama hizi za utandawazi kitu kama hicho kimebakia kama simulizi au hakipo kwa ujumla. Mgawanyo wa shughuli za nyumbani kwetu uliendana na kundi rika na baadhi ya kazi zilizokuwa zikifanywa na familia yetu ni pamoja na ukulima na ufugaji. Kutokana na juhudi binafsi zilizofanywa na baba yetu za kujitaftia mali hasa katika mashamba ya chai huku Tanga, nyumbani kwetu hapakukosekana mahitaji ya lazima kama vile chakula, maradhi na mavazi. Tuliishi kikoa kwa maadili ya upendo na mshikamano. Katika vitu ambavyo baba yetu hakuthubutu kuvifanyia ajizi juu yetu ni pamoja na suala zima la kupata elimu kwa kiwango chochote kile. Miongoni mwa watoto waliobahatika kutumia pesa ya baba yetu kwa uzuri kutokana na suala la elimu ni mimi Davis mwana wa Sikitiko.

********

Niliamshwa na kelele za gereji uchwara zilizojipanga kwenye makazi ya watu na kusababisha kero kwa watu ya kupata raha ya usingizi kwa wingi wa kelele hizo. Ikiwa ni muendelezo wa likizo yangu ambayo sikupenda hata kukanyaga nyumbani kwetu ili niungane na ndugu zangu katika kusherekea sikukuu ya Krismasi na Sherehe za kuadi mwaka yaani mwaka mpya. Nilichukua mswaki wangu nikautia dawa ya meno kisha nikaelekea maliwatoni kuufanyia usafi mwili wangu kwa ujumla. Nikiwa bafuni huku mlango ukiwa wazi, nilikipokea kivuli kilichoambatana na manukato toka nyuma yangu jambo ambalo lilisababisha tundu za pua yangu kupooza kwa muda kwa kutoinusa vema aina ya manukato iliyopokea huku presha ya mapenzi au Fumanizi la Mapenzi ikinipanda kwa kasi ya ajabu kana kwamba ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kuitembelea bustani ya raha iletayo karaha endapo hutaitendea haki katika kuihudumia. Kupitia kioo kilichokuwa mule bafuni chenye ukubwa wa kutosha kilijitokeza kivuli halisi cha kimwana Lulu kama taswira akiwa mtupu mithili ya kichanga kilichopokelewa na wakunga katika chumba maalumu cha kukaribishia watoto wachanga wanaotafuta usajili wao wa awali hapa duniani. Kioo hakikunidanganya kwani Lulu aliingia bafuni kwa mwendo wa kunyata mithili ya kinyonga anyemeleapo mawindo yake ya wadudu huku macho yake ya duara yaliyozungukwa na muonekano wa huba yakijionesha wazi wazi.

********

Kama kuna upendeleo uliowahi kufanywa na Mwenyezi Mungu katika Suala zima la uumbaji kwa watoto wa kike, basi ni miongoni mwa waliopendelewa sifa mubashara za bayana na tafsida. Pia katika ugawaji wa majina wazazi wake hwakukosea kumuita kwa jina la Lulu hata kidogo kulingana na sifa zake. Kama jina lake linavyosadifu thamani ya lulu kama kitu, naye kimwana Lulu thamani yake haikuwa ya kitoto hasa pale walipojipanga wanaume wakware na wenye ukwasi kama kina Davis Sikitiko. Kutokana na uthamani wake kwa wanaume aliweza kuhongwa vitu vya thamani kubwa yakiwemo magari ya kifahari, vitu vya thamani na hata kumilikishwa hati ya viwanja vyenye majumba ya kifahari. Kimwana Lulu ni miongoni mwa watoto wa kike waliojaaliwa muonekano wa kuvutia kwa wanaume marijali na wale wasio marijali . kwa uchache alikuwa ametunukiwa tunu ya uumbaji kwa idara zote zimuhusuzo mtoto wa kike kuanzia chini hadi juu. Alikuwa mweusi wa mng’ao usiohitaji aina yoyote ya mkorogo uliobebwa na uso wa mvuto wenye macho ya kuita hata kama hautaki kuitika. Alisheheni kifua cha kike kilichobeba chuchu mchomoko zenye ujazo wa kumpumbaza mwanaume yoyote yule. Kwa upande wa tumbo alizawadiwa tumbo la shukrani ya siri yaani lile ambalo mtu akiwa na njaa au ameshiba halijulikani labda kwa wataalamu wa “totozi” kama mimi ….na matumbo kama haya huzawadiwa kwa watoto wa kike wachache sana. Wasifu wa matumbo hayo huwa yamebeba tumbo la mviringo lililozungukwa na vimalaika vya nywele mithili ya nywele za mtoto mchanga. Licha ya hivyo matumbo hayo huwa na kitovu kilichozama ndani chenye mfereji alama uelekeao kwenye kisiwa cha huba ya malavidavi. Mgawanyo wa chini na juu kwa kimwana Lulu umekwenda sambamba kwa upande wa kati kuzawadiwa hipsi asilia zilizomfanya azidi kuwa kivutio kwa wanaume Washongo. Kwa uzuri wa kimwana Lulu, inasemekana alishawahi kumsababishia rubani wa shirika moja la ndege hapa Tanzania kufukuzwa kazi mara baada ya kushusha ndege Lushoto badala ya kiwanja cha Lindi. Hii ilitokana na kulikariri jina la Lulu na uzuri wake.

********

Kimwana Lulu alijiunga nami bafuni kisha tukaendeleza michezo ya kumwagiana vimaji vya kichokozi vya asubuhi huku kila mmoja wetu akimtamani mwenzake. Kilichotawala humo bafuni vilikuwa ni vikofi mahaba, mbadilishano wa ladha ya chumvi chumvi kupitia njia ya kunyonyana ndimi na kuandaa mazingira ya kuupasha moto mwamba ili mtarimbo upenye vizuri katika kuyabandua matabaka ya miamba ili vito vya lulu vipatikane kwenye mwamba husika. Kazi ya kuitafuta lulu ilianza kwa mwendo wa taratibu hadi pale ambapo mtarimbo uligusa tabaka la mwamba geu ndipo kasi ilipoongezeka …………..Sauti za mlio wa mtarimbo juu ya mwamba ndiyo iliyokuwa imetawala huku mwangwi nao ukienda sambamba na mapigo hayo ukimaanisha kuwa mtarimbo haujakosea vijia na muda si mrefu lulu itakuwa hadharani huku mtarimbo ukisafishwa kwa vimiminika vya maji kutoka kwenye matabaka ya miamba ya mahaba iliyozungukwa kwa vinyasi chupuki vilivyotulia mithili ya zile zinazosubiri kumwagiliwa na mvua za kwanza za vuli.

====>>Itaendelea wiki ijayo...

Usiikose SEHEMU YA 02>>> ya Riwaya hii ifikapo jumatatu ya wiki inayofuata, na utaipata hapa Zero Degree pekee. 
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 01 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 01 Reviewed by Zero Degree on 6/02/2017 02:39:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.