Ewura yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ambaye ameeleza kwamba bei hiyo ni kwa upande wa Tanzania bara huku akiongzea kwamba punguzo hilo ni kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika bandari ya Dar es Salaam ambapo watumiaji wa bandari ya Tanga bei itaongezeka.
Bei ya petroli imepungua kwa Shilingi 88 kwa lita (sawa na asilimia 3.8), dizeli Shilingi 61 kwa lita (sawa na asilimia 2.75) na mafuta ya taa imeongezeka kwa Shilingi 2 kwa lita (sawa na asilimia 0.09). Aidha, bei ya jumla ya petroli imepungua kwa Shilingi 100.91 kwa lita (swa na asilimia 4.58), dizeli Shilingi 73.71 kwa lita (sawa na asilimia 3.52) na mafuta ya taa ni Shilingi 10.49 kwa lita (sawa na asilimia 0.51).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mafuta yanayopitia bandari ya Tanga bei yake kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka kwa asilimia 0.14 kwa petroli na asilimia 0.71 kwa dizeli huku bei ya jumla ikipungua kwa Shilingi 9.8 kwa lita (sawa na asilimia 0.46) kwa petroli na Shilingi 1.9 kwa lita (sawa na asilimia 0.1) kwa dizeli.
Ewura imesema kutokana na kupungua kwa mafuta ya taa katika bandari, huku ikiwashauri watumiaji wa mafuta hayo kwa mikoa ya Nyanda za Juu ambao hutumia bandari hiyo, kuchukua bidhaa hiyo katika bandari ya Dar es Salaam kwa bei iliyoelekezwa.
Ewura yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta
Reviewed by Zero Degree
on
5/01/2018 12:20:00 PM
Rating: