Loading...

Mashabiki Arsenal wanataka mchezaji huyu auzwe kwenye majira ya joto


Mashabiki wa Arsenal wamepeleka hisia zao kwenye ukurasa wa Twitter baada ya kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Manchester United kuonyesha ni kiasi gani walivyochukizwa na golikipa wa klabu hiyo, David Ospina.
Raia huyo wa Colombia alikuwa golini katika mechi hiyo na mashabiki wanaamini yeye ndio chanzao cha timu yao kufungwa goli katika dakika za majeruhi na kuwapelekea kupoteza mchezo.

Ospina amekuwa akipewa nafasi ya kulinda mlango kwenye michuano ya vikombe msimu huu lakini amechukuwa nafasi ya Petr Cech kwenye Ligi Kuu wiki za hivi karibuni, ambaye ni majeruhi.
Mashabiki wa Arsenal hawakufurahishwa na kiwangoi chake na wengi wao wanaona hajafikia vigezo vya kuwa golikipa namba moja wa klabu yao.

The Gunners watakuwa wanatazamia kuwa na mwanzo mpya kwenye majira ya joto wakati Arsene Wenger atakapoondoka katika klabu hiyo.
Mashabiki Arsenal wanataka mchezaji huyu auzwe kwenye majira ya joto Mashabiki Arsenal wanataka mchezaji huyu auzwe kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 5/01/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.