Loading...

Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020 itachezwa katika Uwanja huu


Uwanja wa Ataturk, ambao unatumiwa na Istanbul umechaguliwa kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020.

Shirikisho la Soka Ulaya, UEFA limetangaza uamuzi huo kufuatia mkutano wa kamati tendaji mjini Kiev, mji ambao fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu huu kati ya Liverpool na Real Madrid itachezewa.

Liverpool wanaziona habari za Alhamisi ya leo kama bahati nzuri kwao, kwani Istanbul ilikuwa ndio sehemu ambayo Liverpool walifanikiwa kushinda taji la michuano hiyo mwaka 2005.

Liverpool walifurahia usiku wa kihstoria mjini Istanbul mwaka 2005
Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu 76,000 ulitumika kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyomshuhudia Liverpool akionyesha maajabu kwa kurejea kutoka kufungwa mabao 3-0 na kushinda fainali ya michuano hiyo kwa mikwaju ya penalti dhidi ya AC Milan mwaka huo.

UEFA wamekuwa chini ya msukumo mkubwa kuhakikisha kuwa miji inayoteuliwa kuwa mwenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa ina hoteli na viwanja vya ndege vya uhakika vinacyoweza kumudu mahitaji ya mashabiki, wajumbe na wandishi wa habari kwa ajili ya mchezo mkubwa zaidi wa mpira wa miguu kwa ngazi ya vilabu.

Fainali ya msimu ujao itachezwa kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano unaotumiwa na Atletico Madrid, ambao unaweza kubeba watu 67,000.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020 itachezwa katika Uwanja huu Fainali ya Ligi ya Mabingwa 2020 itachezwa katika Uwanja huu Reviewed by Zero Degree on 5/24/2018 01:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.