Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 24 Mei, 2018

Robert Lewandowski
Manchester United wamejiunga na mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski, hivyo watakabiliana na ushindani kutoka Chelsea na PSG.
 
Bayer Leverkusen wamethibitisha kuwa golikipa wa klabu hiyo, Bernd Leno ataondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto. (Kicker)

Mshambuliaji wa Chelsea amehusishwa na uhamisho kwenda AC Milan, lakini wawakilishi wake walionekana wakifanya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Juventus. (Calciomercato)

Arturo Vidal ni yuko kwenye rada za Manchester United, licha ya kuwa na mkataba na klabu ya Bayern Munich hadi mwaka 2019. (SportBild)

Villareal wanakaribia kumnasa nyota anayelengwa na klabu ya Newcastle United, Toko Ekambi na wanaweza kumsajili mshambuliaji huyo wa Angers kwa pauni milioni 15.76. (Marca)

Napoli wamethibitisha kumteua Carlo Ancelotti kuwa meneja wao mpya wa klabu hiyo.

Simon Mignolet amesema kuwa hataki uvumi unaoenea juu ya hatima yake katika klabu ya Liverpool usivuruge maandalizi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.

West Ham wamethitisha kwamba James Collins na Partrice Evra wataondoka mikataba yao itakapoisha tarehe 30 Juni, 2018.

Fred
Manchester United wakaribia kukamilisha dili la uhamisho wa kiungo wa klabu ya Shakhtar Donetsk na timu ya taifa ya Brazil, Fred.

Kiungo wa Uhispania, Andres Iniesta amejiunga na klabu ya Vissel Kobe ya Japan.

Derby hawana mpango wa kuharakisha mchakato wa kusaka mkufunzi mpya atakayekinoa kikosi chao.  

Aston Villa wataanza mazungumzo ya mkataba mpya na beki wa klabu hiyo, Alan Hutton wiki ijayo. (Sky Sports)

Tottenham wameanza mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya uhamisho wa Toby Alderweireld anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 75.

Willian yuko tayari kujiunga na Manchester United, wakati ambapo uwezekano wa yeye kuondoka Chelsea ni mkubwa.

Arsenal wako tayari kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Adrian Rabiot kufuatia kuachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Waamuzi watatu wa Arsenal waliweka bahasha ya kura ya siri ya kuchagua meneja pya - na kura zao zote ziligongana kwa Unai Emery.

Gianluigi Donnarumma
Liverpool wana hamu ya kumpata golikipa wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma kwenye majira ya joto.

Manuel Pellegrini ana hamu ya kumnasa golikipa wa Reims, Edouard Mendy ili kuanzisha utawala wake kama meneja wa West Ham. (Mirror)

Arsenal wako tayari kwa kumnyakuwa nyota wa klabu ya Nice, Jean-Michael Seri kwenye usajili wa majira ya joto.

Nyota wakubwa wa Everton wako tayari kuondoka katika klabu hiyo kutokana na mgogoro mkubwa katika chumba cha kubadilishia nguo unaomuhusisha Tom Davies na Oumar Niasse.

Kiungo anayewindwa na Manchester City, Jorginho atafanya mazungumzo na klabu ya Napoli wiki ijayo.

Meneja wa klabu ya West Ham, Manuel Pellegrini anataka kumfanya golikipa wa Chelsea, Willy Caballero kuwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili kwenye majira ya joto.

West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 1.2 kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Derby County, Luke Thomas. (Sun)

Graham Potter amekanusha taarifa zinazodai kwamba atakuwa meneja mpya wa Swansea.

Mohamed Salah
Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah ataendelea na mfungo wake wa Ramadhani kama kawaida siku ya Jumamosi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa. (Express)

Southampton hawatapewa bonasi yoyote ikitokea kama mmoja wa waliokuwa wachezaji wao ataisaidia Liverpool kushinda Taji la Ligi ya Mabingwa. (Times)

John Terry anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa miezi 12 kama Aston Villa itapanda daraja. Mkataba huo utakuwa na kipengele kitakachomfanya akose mechi zote dhidi ya klabu yake ya zamani, Chelsea. (Telegraph)

Mmoja wa wamiliki wa klabu ya West Ham, David Gold amethibitisha kuwa klabu itamuunga mkono meneja mpya, Manuel Pellegrini na kufanya matumizi ya fedha yatakayovunja rekodi ya klabu kwenye usajili wa majira ya joto.

Nyota wa timu ya taifa ya Uingereza wanaochezea kwenye vilabu vilivyoshuka daraja wanahaha kusaka vilabu vipya vya kuchezea ili kujihakikishia wanendelea kubaki kwenye mipango ya Gareth Southgate.

Paul Robinson anaamini Joe Hart ana uwezo wa kurejea kwenye kiwango chake cha awali kilichompa nafasi ya kushiriki mechi 75 na timu ya taifa ya Uingereza, na hivyo arejee kwenye nafasi yake ya kawaida kama golikipa namba moja wa timu ya taifa. (Daily Mail)

Maurizio Sarri amekataa ofa ya pauni milioni 5.2 kwa mwaka akiwa kama meneja wa klabu ya Zenit St Petersburg, akizipa kipaumbele mbio za kuwania kibarua cha kuinoa Chelsea.

Massimiliano Allegri angaweza kuwa meneja mpya wa klabu ya Arsenal kama Arsene Wenger angeachia madaraka mwaka mmoja kabla.

Marco Silva
Meneja mpya wa Everton, Marco Silva anakaribia kukutana na mkurugenzi mpya wa kandanda wa klabu hiyo, Marcel Brands wiki hii. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 24 Mei, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 24 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/24/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.