Loading...

Lionel Messi aandika rekodi mpya barani Ulaya

Lionel Messi
Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi jana usiku amemaliza mchezo wake wa mwisho wa La Liga kwa msimu huu kwa kutwaa tuzo ya kiatu cha dhahabu barani Ulaya.

Messi amemaliza msimu wa mwaka 2017/18 akiwa na magoli 34 na kuwa mchezaji mwenye magoli mengi katika ligi zote kubwa barani Ulaya akimuacha mshindani wake Mohamed Salah wa Liverpool kwa magoli mawili (32) .

Hii ni mara ya tano kwa mshambuliaji huyo Muajentina kuchukua tuzo hiyo na kuweka rekodi ya mchezaji wa kwanza barani Ulaya kuchukua kwa wingi tuzo hiyo kwa muda wote.

Kwenye mchezo huo wa jana Barcelona waliibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Real Sociedad na goli hilo pekee la ushindi lilifungwa na Phillippe Coutinho.


Lionel Messi aandika rekodi mpya barani Ulaya Lionel Messi aandika rekodi mpya barani Ulaya Reviewed by Zero Degree on 5/21/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.