Serikali yanunua tiketi 10,000 kuiona Taifa Stars dhidi ya Madagascar
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Ndg. Gerson Msigwa, amesema kuwa, Serikali imenunua tiketi 10,000 zenye thamani ya Shilingi milioni 20, kwa ajili ya mashabiki kuingia uwanjani kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wake dhidi ya Madagascar, mchezo utakaochezwa leo Agosti 9, 2025 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Msigwa amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam, na kuwahamaisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars ili iendelee kufanya vizuri katika michuano ya CHAN 2024 inayoendelea.
Serikali yanunua tiketi 10,000 kuiona Taifa Stars dhidi ya Madagascar
Reviewed by Zero Degree
on
8/09/2025 12:41:00 PM
Rating:
