Loading...

Mtoto wangu na wa Lukuvi, hawawezi kupata mkopo - Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuna vigezo muhimu ambavyo huzingatiwa ikiwa ni pamoja na kuangalia hali ya familia ya muombaji.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 02, alipokua akihutubia wanafunzi na uongozi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa na kuongeza kuwa kwa familia ambazo zinauwezo hasa viongozi hawana sifa za kupata mkopo hata ingekua ni mtoto wake.

“Hiki sio kitu kidogo, kwa mwaka unatoa bilioni 427, kwa nchi masikini kama Tanzania na unapotoa mkopo ni lazima pawepo na utaratibu na taratibu hizo zinaendeshwa na watu, na ndiyo maana mtoto wangu mimi hawezi kupata mkopo, mtoto wa( William) Lukuvi, mtoto wa Profesa haitaji kupata mkopo, mtoto wa mkuu wa mkoa hatakiwi kupata mkopo” alisema Rais Magufuli

Rais Magufuli amedai kwamba wanafunzi wa elimu wa juu wanaonufaika na mkopo kwa sasa ni zaidi ya 130,000 ambapo serikali imetoa bilioni 427.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amekiri serikali kukumbwa na changamoto ya kubaini wanafunzi hewa wa elimu ya juu zaidi ya 3500 katika orodha ya wanufaika na mikopo.
Mtoto wangu na wa Lukuvi, hawawezi kupata mkopo - Rais Magufuli Mtoto wangu na wa Lukuvi, hawawezi kupata mkopo - Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 5/02/2018 03:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.