Loading...

Mwanafunzi ajitosa kueleza shida ya shule yao kwa Rais Magufuli, amwagiwa mamilioni


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alipokua akiendelea na ziara yake mkoani Morogoro akielekea Kilombero amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’ula ambapo alisimama na kuzungumza na wananchi.

Baada ya kufanya mazungumzo na wananchi aliuliza kama kuna mwalimu au mwanafunzi aeleze changamoto waliyonayo, hatimae mwanafunzi wa Kidato cha kwanza wa shule ya Sekondari Mang’ula aliyejitambulisha kwa jina Mlindoka Msangi alisema kuwa shule hiyo ina changamoto ya vyoo.

Rais Magufuli alitoa na kumkabidhi mwanafunzi huyo Milioni tatu kwaajili ya ujenzi wa vyoo na kumkabidhi mtoto huyo kwa askari polisi na huku akimwagiza kuhakikishe fedha hizo zinafika shuleni katika shule hiyo.

Hata hivyo Rais Magufuli aliwataka nao wachangie fedha za ujenzi wa vyoo hivyo ili changamoto hiyo iweke kuisha.
Mwanafunzi ajitosa kueleza shida ya shule yao kwa Rais Magufuli, amwagiwa mamilioni Mwanafunzi ajitosa kueleza shida ya shule yao kwa Rais Magufuli, amwagiwa mamilioni Reviewed by Zero Degree on 5/05/2018 10:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.