Loading...

PSG yashauriwa kumsajili nyota huyu wa Real Madrid

Thiago Motaa anaamini nyota wa klabu ya Real Madrid, Toni Kross ataifaa Paris Saint-germain
Thiago Motta alijiunga na Paris-Saint Germain akitokea Inter Milan kwa ada ya uhamisho ya pauni 8.77 mwaka 2012. Amekuwa mchezaji mwenye umuhimu kwa klabu tangu wakati huo na kujiendeleza hadi kufikia hatua ya kujumuishwa kwenye orodha ya viungo bora zaidi kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa.

Muitaliano huyo alicheza mechi 27 katika klabu hiyo kwenye michuano yote msimu huu na kuisaidia timu kushinda taji la Ligue 1. Alistaa mwishoni mwa msimu na atakuwa msimamizi wa kikosi cha PSG U-19 msimu ujao.

Mabingwa hao wa Ligue 1 wanatarajiwa kuongeza nguvu mpya kwenye kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, huku kushinda taji la Ligi ya Mabingwa ikiwa ndio kipaumbele chao. Motta ameishauri timu kumsajili nyota wa Real Madrid, Toni Kroos kwenye dirisha la usajili wa majira ya joto na anaamini Mjerumani huyo anaweza kuwa na faida kubwa kwao.

Raia huyo wa Ujerumani alijiunga na vigogo hao wa La Liga akitokea Bayern Munich miaka minne iliyopita na amekuza kipaji chake hadi kufikia hatua ya kuwa miongoni mwa viungo bora duniani. Ameshinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na moja la La Liga tangu ajiunge na klabu hiyo.

Kiungo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani, Toni Kross
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 alikuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Real Madrid msimu huu, akifunga mabao 5 na kutoa 'assist' 7 kwenye mechi 27 za La Liga na kuisaidia timu kushinda taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa dhidi ya Liverpool.

Kwa mujibu wa taarifa ya Goal, Motta aliiambia Le Parisien: “Binafsi, ningependelea kumuona Toni Kroos akiwa PSG.”

“Naweza pia kucheza kwenye nafasi za juu zaidi, lakini kwa mtindo ambao unaifaa PSG, ni wa kipekee.

“Ni mchezaji anayenivutia kwa sana na kwa muda mrefu. Anaweza kucheza katika nafasi tatu za kiungo na zaidi hasa mbele ya safu ya ulinzi.”
PSG yashauriwa kumsajili nyota huyu wa Real Madrid PSG yashauriwa kumsajili nyota huyu wa Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 5/31/2018 03:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.