Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 12 Mei, 2018

Harry Kane
Arsene Wenger amewaambia Tottenham kuwa wanaweza kulazimika kumuuza Harry Kane ili kupata fedha ya kulipia uwanja wao mpya.

Romelu Lukaku bado anapigania kuwa fiti kwa ajili ya fainali ya FA Cup kati ya Manchester United na Chelsea.

Inadaiwa Arsenal walimpa Pierre-Emerick Aubameyang pauni milioni 15.5 inje ya fedha ya usajili. (Sun)

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, Alexis Sanchez anaweza kuingiza karibu pauni milioni 25 kwa mwaka katika klabu ya Manchester United.

Muda wa Wayne Rooney nchini Uingereza unaweza kuwa umeisha baada ya kuwa ameachwa nje ya mchezo wa mwisho wa Everton msimu huu kufuatia majeraha yake ya goti.

David Wagner atajadili juu ya hatima yake katika klabu ya Huddersfield wiki ijayo baada ya kuiongaza klabu hiyo hadi kwenye nafasi salama kwenye msima wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Wachezaji wa West Ham wanatarajiwa kutokuwa na la kusema kama David Moyes anabikia au anaondoka katika klabu hiyo.

Cardiff City inataka kumsajili kiungo wa Rangers, Josh Windass.

Bayern Munich wanafuatilia maendeleo ya winga wa klabu ya Chelsea, Kenedy, huku winga wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic pia akiwa kwenye malengo yao. (Daily Mail)

Liverpool wanahofia mshambuliaji wao chipukizi, Rhian Brewster anaweza kuvutiwa na uhamisho kwenda Bundesliga.

Jose Mourinho analenga kumsajili straika wa Ajax, Justin Kluivert kwenye majira ya joto, huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 19 akionekana anapendelea uhamisho kwenda Old Trafford. (Guardian)

Sam Allardyce atakutana na Mwenye hisa mkuu wa Everton, Farhad Moshiri wiki ijayo kutafuta utatuzi wa hatima yake katika klabu hiyo. (Telegraph)

Manuel Pellegrini
Manuel Pellegrini yuko kwenye orodha fupi ya wakufunzi wanaowaniwa na klabu ya West Ham kama haitafikia makubaliano na David Moyes.

Mo Salah alitumia miezi sita pekee kupokea bonasi ya pauni milioni 2.5 kwenye mkataba wake kwa kufunga magoli na kutoa 'assist'.

Chipukizi wa Uingereza, Nathaniel Chalobah anatarajiwa kurejea katika kikosi cha Watford kwenye mechi yao dhidi ya Manchester United.

Mashabiki wa Uingereza wanaelekea katika nchi za ukanda wa Bahari ya Baltic kama vile Latvia, Estonia na Poland ili kuepukana na mfumko wa bei za Hoteli nchini Urusi kwenye Kombe la Dunia. (Mirror)

Mwenye hisa mkuu wa Everton, Farhad Moshiri anatazamia kuongeza hisa zake za umiliki katika klabu hiyo hadi karibia na asilimia 60 kwa kununua hisa za is mwenyekiti msaidizi, Jon Woods.

Mazungumzo juu ya mkataba wa Ben Mee katika klabu ya Burnley yamevunjika na inaonekana beki huyo wa kati wa klabu hiyo anaweza kuuzwa kwenye majira ya joto kwa sababu klabu hiyo haiko tayari kutimiza mahitaji yake ya mkataba mpya wenye thamani ya pauni milioni 80,000 kwa wiki.

Wachezaji wa Huddersfield Town wanatarajia kupokea pauni 344,000 kila mmoja kwa kusalia katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Times)

Meneja wa St Mirren, Jack Ross anakiri kuwa anasubiriwa kutoa uamuzi wa hatima yake baada ya kupewa ruhusa ya kufanya mazungumzo na klabu ya Ipswich Town juu ya kibarua cha Ukufunzi. (Record

Darren Moore
Darren Moore atazungumzia juu ya hatima yake katika klabu ya West Brom wiki ijayo. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 12 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 12 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/12/2018 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.