Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 29 Mei, 2018

Riyad Mahrez 
Riyad Mahrez anaonekana kama vile atafanikiwa kukamirisha uhamisho wake wa pauni milioni 75 kwenda Manchester City.

Golikipa wa Man City, Joe Hart amebadilisha mawakala, ikiwa ni mkakati wa kusaka uwezekano wa kurejea kwenye kiwango chake cha zamani.

Liverpool watajaribu kuishawishi Roma na ofa itakayoweka rekodi ya dunia kwa ajili ya golikipa wao, Alisson Becker.

West Ham wanakaribia kumteua Mario Husillos kuwa mkuu wao mpya wa kitengo cha ajira.

Luke Shaw yuko tayari kubakib Manchester United na kumaliza mkataba wake.

Zaidi ya watu 370,000 wamesaini ombi la kuitaka UEFA na FIFA wamwadhibu Sergio Ramos kwa kumuumiza Mohamed Salah. (Daily Mail)

Juventus wanategemea Maurizio Sarri atajaribu kumsajili Higuan kama atakuwa meneja wa Chelsea. (Gazetta dello Sport)

Borussia Dortmund wanataka kumsajili Matthijs De Ligt kutoka Ajax lakini wanakubali kuwa idadi ya vilabu vinavyomfukuzia nyota huyo wa Uholanzi italeta ushindani mkubwa. (Kicker)

Mauro Icard
Juventus wametoa ofa ya pauni milioni 43 pamoja na Gonzalo Higuan kama sehemu ya ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icard.

Napoli wanataka kumfanya kiungo wa klabu ya Real Betis, Fabian Luiz kuwa mchezaji wao wa kwanza kumsajili katika enzi za utawala mpya wa Carlo Ancelotti. (Corriere dello Sport)

Wakala wa Gareth Bale, Jonathan Barnett anatarajiwa kukutana na viongozi wa Real Madrid kujadili juu ya hatima ya raia huyo wa Wales - lakini nyota huyo hatarejea katika klabu ya Tottenham.

Meneja wa klabu ya Ostersunds, Graham Potter amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na Swansea kuhusu kuwa meneja wao mpya.
 
Sevilla wamemteua Pablo Mancin kuwa meneja wao mpya baada ya kuisaidia klabu ya Girona kumaliza katika nafasi ya kumi kwenye msimamo wa La Liga, ambapo ilikuwa mpya kwenye La Liga msimu huu baada ya kupanda daraja mwaka jana.
 
Frank Lampard anakaribia kusaini mkataba wa kuwa meneja mpya wa klabu ya Derby County. (Sky Sports)

Barcelona wamemtaja kiungo wa klabu ya Tottenham kama mtu sahihi wa kuchukua nafasi ya Andres Iniesta. (Sport)

Angel Di Maria anataka kujiunga na klabu ya Atletico Madrid kwenye majira ya joto, huku Diego Simeone akiwa kwenye msako wa mchezaji wa nafasi ya kiungo mwenye kipaji kizuri. (AS)

David Alaba
David Alaba amesisitiza kuwa atakuwa na Bayern Munich msimu ujao na anaamini majadiliano yaliyochapishwa Uhispania yakimnukuu baba yake yalikiwa ni ya kutengeneza. (Sport Bild)

AC Milan wameelezea nia yao ya kutaka kumsajili beki kutoka klabu ya Lyon, Marcelo.
 
Mino Raiola amezitaja Roma na Napoli kama sehemu pekee anazoona kwa mteja wake, Mario Balotelli. (L'Equipe)

Ofa ya pauni milioni 39 iliyotolewa na Manchester City kwa ajili Jorginho ilikataliwa na Napoli, ambao wana matumaini Chelsea atajiunga kwenye mbio hizo kuongeza ushindani kwenye kuwania saini ya kiungo huyo wa Italia.

Adam Lallana amekuwa akitokea mazoezini mapema kwa lengo la kumvutia meneja wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate.

Everton wanatarajia kumteua Marco Silva baada ya kufikia makubaliano kwenye mazungumzo yao na Mreno huyo.

Liverpool wanapigania kukamilisha usajili wa Nabil Fekir, kuondokana na gharama kama itatokea ushiriki wake kwenye michuano ya Kombe la Dunia utaongeza thamani yake maradufu.

Paul Heckingbottom anaweza kufukuzwa kazi kabla hajatimiza miezi minne katika klabu ya Leeds tangu kuteuliwa kwake.

 Joe Bryan
Burnley watamsajili beki wa klabu ya Bristol City, Joe Bryan kwa pauni milioni 6, huku kiungo wa Southampton, Sam McQueen akijiunga na Bristol City. (Mirror)

Gareth Bale ni chaguo la kwanza la Manchester United lakini hata pauni milioni 349 inaweza kuwa ni ghali sana kwao.

Manchester United wanamfuatilia nyota wa klabu ya Aston Villa, Jack Grealish.

Jamie Vardy ameanza mazungumzo ya mkataba mpya wa pauni 120,000 kwa wiki katika klabu ya Leicester.

Wolves wanafanya mpango wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya AC Milan, Andre Silva kwa pauni milioni 27. (Sun)

Vigogo wa FA wameonywa kuwa watakuwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe juu ya mapendekezo ya kuuza uwanja wa Wembley kwa Shahid Khan.

Arsenal wanakaribia kumsajili beki wa klabu ya Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos.

Tottenham wanatafakari kugeuzia nguvu zao kwenye usajili wa winga wa klabu ya Borussia Dortmund, Christian Pulisic. (Telegraph)

Ryan Sessegnon
Ryan Sessegnon atakuwa katika klabu ya Fulham msimu ujao licha ya uvumi unaoenea ukidai kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 18 atajiunga na moja kati ya vilabu vikubwa barani Ulaya. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 29 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 29 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/29/2018 10:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.