Serikali imetoa ufafanuzi kuhusiana na tetesi za ugonjwa wa Ebola kuingia nchini
Serikali imesema ugonjwa wa Ebola haujaingia Tanzania na kwamba imeanza kuchukua tahadhari za kuuzuia kuingia nchini huk ugonjwa huo ukiwa umeripotiwa kujitokeza Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Serikali imesema kuwa moja ya hatua ni kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji mipakani.
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, maendeleo ya jinsia wazee na watoto Dkt Mpoki Ulusubisya amezungumza na waandishi wa Habari, jijini Dar es saaam, akiwataka wananchi kutokuwa na hofu bali wachukue tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo, kwa kuwa hadi sasa hakuna mtu aliyethibitishwa kuugua ugonjwa huo nchini.
“Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jinsia wazee na watoto itaendelea kuchukua hatua zifuatazo ili kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Makatibu Tawala na waganga wakuu wote wa mikoa,” alisema Ulusubisya.
“Aidha taarifa hii itajumuisha ainisho la ugonjwa, lakini fact sheet ya ugonjwa, Muongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli na namna ya kuwahudumia wagonjwa watakao kuwa wamepata changamoto hii.”
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusiana na tetesi za ugonjwa wa Ebola kuingia nchini
Reviewed by Zero Degree
on
5/17/2017 12:08:00 AM
Rating: