Loading...

Guardiola amkejeli Arsene Wenger

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amemtaka Arsene Wemger kuacha maneno badala yake aonyeshe soka uwanjani.

Guardiola alimkajeli Wenger akisema amekuwa akiendekeza malalamiko badala ya kikosi chake kufunga mabao.

Alisema Wenger aache uoga na ajikite kwenye kusakata soka uwanjani kuliko kuzilaumu klabu zingine kwenye Ligi Kuu.

Guardiola aliyatoa maoni hayo baada ya Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhdi ya West Ham.

Alisema, “Nashindwa kuwaelewa hasa makocha wanaozilalamikia klabu. Muulize Wenger hili jambo. Timu zinajipanga kushinda na ndicho zinachokifanya.”

Malalamiko ya Wenger yamekuja kutokana na kuwapo na ushindani mkali wa kumaliza katika nafasi nne za juu. Wenger amezitupia lawama klabu zinazowapa mwanya wapizani wake hao kufunga mabao mengi.
Guardiola amkejeli Arsene Wenger Guardiola amkejeli Arsene Wenger Reviewed by Zero Degree on 5/16/2017 11:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.