Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 14 Mei, 2018
Eden Hazard |
Chelsea wanahofia Eden Hazard anaweza kulazimisha kuondoka kwenda Real Madrid kwenye majira ya joto isipokuwa kama Antonio Conte atatimuliwa.
PSG watajaribu kumsajili Paul Pogba kwenye majira ya joto kama Neymar ataondoka kwenda Real Madrid.
Gary Cahill alidai kuwa Chelsea ilifungwa mabao 3-0 na Newcastle kwa sababu wachezaji walikuwa na mawazo ya fainali ya FA Cup. (Star)
Jose Mourinho anasema kuwa Michael Carrick atakuwa meneja wake msaidizi katika klabu ya Manchester United.
Arsene Wenger amesistiza kwamba Herbert Chapman ni meneja bora zaidi aliyewahi kutokea katika historia ya klabu ya Arsenal. (Sun)
Manchester United wanatarajia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 50 wa beki wa klabu ya Juventus, Alex Sandro baada ya fainali ya FA.
Kalidou Koulibaly |
Arsenal wanatazamia kumsajili beki wa kati kutoka klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly kwa pauni milioni 53.
Everton inakabiliwa na vita ya kumpata meneja, Marco Silva anayedaiwa kuwa chaguo la kwanza la klabu hiyo.
David Wagner alikataa kutoa uamuzi wa uhakika wa hatima yake katika klabu ya Huddersfield kama meneja. (Mirror)
Arsene Wenger haamini kama yuko tayari kuwa mkufunzi katika klabu nyingine dhidi ya Arsenal, baada ya kuwa ameisimamia klabu hiyo kwa mara ya mwisho jana Jumapili. (Independent)
Meneja mpya wa Rangers, Steven Gerrard aliwashuhudia Celtic wakinyanyua Kikombe cha Ligi Kuu na kuwaonya kuwa siku za kubeba ubingwa kiurahisi zimekwisha. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 14 Mei, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
5/14/2018 01:40:00 PM
Rating: