Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 28 Mei, 2018

Alisson Becker
Liverpool wanafanya mpango wa kumsajili golikipa wa klabu ya Roma, Alisson baada ya Loris Karius kufanya makosa yaliyoigharimu timu kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.


Gareth Bale hatalengwa na vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza pekee kama ataamua kuondoka Real Madrid, huku vigogo wa Bundesliga, Bayern Munich pia wakiwa na hamu ya kumnasa nyota huyo kutoka Wales. (Telegraph)

Manchester United na Chelsea wote wanaangalia maendelea ya sakata la Gareth Bale katika klabu ya Real Madrid wakiwa na nia ya kumsajili.

Mmiliki wa klabu ya Derby County, Mel Morris amesema utawala mpya unakaribia, kuongeza matumizi katika klabu hiyo baada ya kushindwa kupanda daraja. (Daily Mail)

Washauri wa Gareth Bale watakutana na rais wa Real Madrid, Florentino Perez ndani ya siku nne zijazo, wakati ambapo nyota huyo anatafakari kuhusu hatima yake, huku kukiwa na madai kwamba huhusiano wake na Zinedine Zidane sio mzuri.

Frank Lampard anaweza kujua itakapofika siku ya Jumatatu, kama Derby County wamemteuwa kuwa meneja wao mpya au la.

Lyon wameeleza nia yao ya kutaka kumsajili beki wa klabu ya Crystal Palace, Mamadou Sakho.

Gerard Deulofeu
Watford wana matumaini ya kufanikiwa kumsajili Gerard Deulofeu kwa mkataba wa kudumu kutoka Barcelona. (Times)

Timu mpya kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao, Cardiff City wanatafakari namna ya kumnasa mshambuliaji wa Watford, Andre Gray.

Ofa ya mkataba mpya unaoambatana na punguzo la mshahara ambao Crystal Palace wamempa Yohan unaweza kupelekea kiungo huyo akaamua kutimkia Marseille. (Mirror)

Real Madrid watahitaji kiasi cha pauni milioni 200 kutoka kwa timu itakayotaka kumsajili Gareth Bale kwenye majira haya ya joto.

Eden Hazard anaunga mkono Chelsea kutaka kumpa kibarua Maurizio Sarri katika klabu yake baada ya kuongea na Dries Mertens, kwa mujibu wa taarifa zilizotoka nchini Italia. (Star)

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis ameikataa ofa ya kwanza ya Chelsea ya pauni milioni 3.5 kwa ajili ya meneja wa Maurizio Sarri, kiasi ambacho kinafikia nusu ya pauni milioni 7 ambazo ndio fedha zainazotakiwa ili kuvunja mkataba wake na klabu hiyo ya Serie A. (Express)

Nottingham Forest wanaweza kumuuza Barrie McKay kwenda Olympiakos ya Ugiriki, ikiwa ni mkakati wa kupunguza matumizi makubwa ya fedha.

Mkurugenzi mtendaji wa Hirbenian, Leeann Dempster ameipotezea nafasi ya kujiunga na Plymouth Argyle. (Record)

Jack Grealish
Swansea, West Brom na Stoke City wote wangependelea kuona kiungo wa klabu ya Aston Villa, Jack Grealish yuko kwenye vikosi vyao msimu ujao. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 28 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 28 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/28/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.